Habari kwa Ujumla

Rais mteule wa UNGA74 ataja vipaumbele vyake

Rais mteule wa Baraza Kuu la Umoja wa Umoja wa Mataifa Balozi Tijjani Muhammad-Bande ametaja vipaumbele vyake vitatu kuwa ni umaskini, elimu bora na ujumuishaji wa kila mtu. 

Sauti -
1'55"

OCHA yatoa wito wa kuimarishwa kwa ufadhili kwa ajili ya CAR

Mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Denise Brown amesema mapigano katika mji wa kasakzini Mashariki mwa nchi hiyo wa Birao, jimbo la Vakaga ,yamesababisha janga kwa wakazi na ni ukiukaji wa haki za binadamu.

Sauti -
1'44"

Dunia yaadhimisha siku ya kulinda wagonjwa kutokana na madhara wakati wa matibabu

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu madhara ya kiafya wanayopata wagonjwa wakiwa wanapata matibabu kwenye vituo vya afya, shirika la afya ulimwenguni , WHO linataka hatua zaidi zichukuliwe kulinda wagonjwa. 

Sauti -
1'26"

Swali la mwanamke aliyebakwa na wanaume 17 ni ishara ya hatua zinazohitajika

Mmoja wa wanawake waliobakwa mara kadhaa na magenge ya wahalifu huko Sudan Kusini amehoji ni hatua gani zitachukuliwa na kamisheni hiyo na jamii ya kimataifa ili kumnusuru yeye na wanaweke wengine waliokumbwa na madhila kama hayo huko Bentiu.

Sauti -
1'50"

Umoja wa Mataifa waungana na dunia kuadhimisha siku ya kulinda tabaka la ozoni

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema dunia inapojikita katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi basi isipuuze tabaka la Ozoni na kuwa na tahadhari ya tishio kubwa linalosababishwa na matumizi haramu ya gesi zinazotoboa tabaka la Ozoni au chlorofluorocarbons.“uta

Sauti -
2'22"

Vijana Kenya wajiandaa ujumbe wao katika mkutano wa hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi

Huku dunia ikikumbwa na changamoto zinazotakana na mabadiliko ya tabianchi harakati zinafanywa kuweza kukabiliana na athari zozote ambazo zinaweza kuibuka siku za usoni.

Sauti -
2'17"

UNESCO yaonya kuwa bila hatua za haraka watoto milioni 12 hawatowahi kutia mguu shuleni

Takwimu mpya zilizochapishwa leo na kitengo cha takwimu cha shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCOkuhusu Watoto wasiohudhuria shule zinaonyesha kwamba hakuna hatua yoyote iliyopigwa au kuna hatua ndogo sana ilipyopigwa kwa zaidi ya muongo mmoja.

Sauti -
2'48"

Ili Afrika izifikie SDGs kwa ubora, inabidi tuanze kukusanya takwimu zetu sisi wewe-Isaya Yunge

Ili nchi za kiafrika ziweze kufikia kwa ubora malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, inazipasa nchi hizo zibuni teknolojia zao wenyewe zitakazosaidia kukusanya takwimu za kijamii badala ya kutegemea data na mipango kutoka nje.

Sauti -
6'

Kenya yazidua chanjo ya malaria, ugonjwa unaoua mtoto mmoja kila baada ya dakika mbili

Shirika la afya duniani WHO limeipongeza serikali ya Kenya kwa kuzindua leo chanjo ya kwanza duniani dhidi ya malaria katika Kaunti ya Homa Bay, magharibi mwa Kenya. 

Sauti -
2'31"

13 Septemba 2019

Katika jarida la kina leo hii Flora Nducha anakuletea

-Kenya imezindua rasmi chanjo ya kwanza ya malaria iliyo kwenye majaribio, ugonjwa ambao hukatili maisha ya maelfu ya watu kila mwaka.

Sauti -
10'47"