Habari kwa Ujumla

Sintosahau nilichokishuhudia kambini Bangladesh:Mkimbizi Asma

Kutana na Asma binti wa miaka 9 mkimbizi kutoka Myanmar ambaye sasa anaishi kwenye kambi ya wakimbizi wa Rohingya ya Katupalong nchini Bangladesh. Anakumbuka alichokishuhudia walipowasili kambini hapo . Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

Sauti -
1'47"

Mkimbizi kutoka Syria awa baraka kwa wenyeji wake Ufaransa

Mkimbizi raia wa Syria ambaye hivi sasa anaishi Ufaransa, amejizolea sifa kwa kuandaa chakula kwa ajili ya kuwasambazia wafanyakazi walioko katika mstari wa mbele wa kupambana na janga la COVID-19 katika nchi yake mpya.Hilda Phoya anafafanua zaidi

Sauti -
1'56"

Hatua za kimataifa zahitajika kuzuia kusambaa kwa mafua ya nguruwe:FAO

Shirika la afya ya wanyama duniani OIE na shrika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo

Sauti -
2'4"

Tusimamie maadili ya Mandela na kuziba pengo la usawa, tukimuenzi: UN

Katika kuelekea siku ya kimataifa ya Nelson Mandela hapo Jumamosi Julai 18, siku ya kuzaliwa kwa mwanaharakati huyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ni muhimu kumuenzi kwa kupigania maadili yake kama kuziba pengo la usawa. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

Sauti -
3'36"

Ziwa Albert lafurika, wakazi wahaha kujinusuru, COVID-19 yazidisha machungu

Wakazi wa maeneo yanayozunguka Ziwa Albert nchini Uganda, wameomba serikali ichukue hatua kuwanusuru na janga la kufurika kwa maji ya ziwa ambalo sasa limesababisha nyumba zao kutwama kwenye maji, huku huduma muhimu za kijamii na kiuchumi zikizamishwa kwenye maji.

Sauti -
5'51"

UNICEF na wadau wanusuru watoto na unyafuzi Madagascar

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linashirikiana na serikali ya Madagascar ili kunusuru watoto waliokumbwa na utapiamlo ulio

Sauti -
1'44"

FIB ya MONUSCO yachukua hatua kuimarisha ulinzi Matembo na Ngadi, DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB, cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo,

Sauti -
3'11"

Kuwa kinyozi ni talanta yangu:Mkimbizi Tekla

Kutana na mkimbizi Tekla kutoka Eritrea ambaye umri wake ni miaka 15, safari ya kwenda kusaka maisha Ulaya iliishia mahabusu Libya na baada ya kuokolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi

Sauti -
2'8"

Nchini Tanzania, UNCDF yachochea maendeleo mji wa Kibaha

Mtaji kutoka shirika la maendeleo ya mitaji la Umoja wa Mataifa, UNCDF kwa halmashauri ya mji wa Kibaha mkoani Pwani nchini Tanzania umewezesha ujenzi wa kituo kipya cha mabasi yaendayo mikoani na hivyo kuchochea maendeleo si tu ya jamii bali ya mkoa husika. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.

Sauti -
2'34"

IOM inasema wahamiaji sio wasambaza COVID-19 ni wapambana na COVID-19

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limesema wahamiaji katika sehemu mbalimbali duniani wamekuwa wakinyanyapaliwa kama waeneza virusi vya janga la corona au COVID-19 suala ambalo ni kinyume na hali halisi.

Sauti -
2'