Umoja wa Mataifa unaendelea kufuatilia kwa karibu hali inayotia hofu kubwa Kaskazini Magharibi mwa Syria kufuatia taarifa kwamba askari kadhaa wa Uturuki wameuawa kwenye shambulio la anga. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Kuelekea jumapili hii ya tarehe Mosi mwezi Machi ambayo dunia inaadhimisha siku ya kupambana na ubaguzi dhidi ya wanawake na wasichana, shirika la Umoja wa Mataifa linalopambana na Virusi Vya UKIMWI, VVU na UKIMWI,
Huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hakuna kisa chochote cha Ebola kilichoripotiwa katika siku 7 zilizopita, na hii ni mara ya kwanza tangu mlipuko wa Ebola mwezi Agosti mwaka 2018 nchini humo.
Nchini Ujerumani, mwanamke mmoja mkimbizi kutoka Syria ametumia stadi zake za mapishi ya vyakula vya kwao na kujikuta anafungua mgahawa unaotoa huduma kwa watu mashuhuru akiwemo Kansela wa nchi hiyo ya Ulaya Angela Merkel.
Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limezindua Apu mpya ya simu za rununu ijulikanayo kama “Community Response App” ambayo inaweza kutumika kokote duniani kuwawezesha wanaosimulia hadithi zao kufanya maamuzi kuhusu matumizi ya taarifa zao binafsi, kulikoni?
Bodi ya kimataifa ya kuzuia madawa ya kulevya INCB imezitaka serikali kuanzisha mifumo ya kitaifa ya data ili kufuatilia mwelekeo wa matumizi ya madawa yenye uraibu miongoni mwa vijana.
Wakati Sudan kusini ikiendelea kupambana kuimarisha amani, wakazi wa eneo la Nzara wamekumbwa na janga la moto wa nyika ambao umeteketeza takribani ardhi yenye ukubwa wa maili tano za mraba katika jimbo la Equatoria Magharibi na kuwaacha mamia ya watu bila makazi, umesema mpango wa Umoja wa Mata
Shirika la afya ulimwenguni, WHO limesema kuwa changamoto kubwa hivi sasa katika kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona au COVID19, ni nchi nyingine zenye wa