Vifo milioni 9 vinaweza kuzuilika kwa kuimarisha juhudi za kukabiliana na homa ya kichomi miongoni mwa watoto, na magonjwa mengine kwa mujibu wa ripoti ya utafiti iliotolewa leo wakati wa kuanza kwa kongamano la kwanza kuhusu homa ya kichomi miongoni mwa watoto mjini Barcelona nchini Uhispania.