Habari kwa Ujumla

Ukosefu wa elimu watumbukiza wengi kwenye ajira zisizo rasmi- Ripoti

Watu bilioni 2 kote ulimwenguni wanafanya kazi katika sekta isiyo rasmi na idadi kubwa ni katika nchi zinazoendelea na zile zinazoibuka kiuchumi.

 

Sauti -
1'6"

Muziki wa Jazz huleta amani-Hancock

Leo ni siku ya kimataifa ya muzizki wa Jazz, na maadhimisho ya kimataifa mwaka huu yanafanyika St. Petersburg, Urusi.

Sauti -
1'39"

UN na wadau waleta matumaini kwa watoto wakimbizi Rwanda

Watoto wakimbizi nchini Rwanda sasa wanaona nuru katika maisha yao kutokana na ushirikiano kati ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na mfuko wa H&M. 

Sauti -
1'22"

Shambulio la kigaidi Afghanistan laua 14 na kujeruhi Zaidi ya 30: UNAMA

Watu takribani 14 wameuawa hii leo na wengine wapatao 0 kujeruhiwa katika mashambulio mawili ya kujitoa muhanga mjini Kabul Afghanistan.

Sauti -
1'

Watu millioni 15 waliuzwa utumwani zaidi ya miaka 400 iliyopita

Wanafunzi mbalimbali kutoka nchi tofauti duniani wameshiriki katika mdahalo kupitia video kama sehemu  ya kuwaenzi wahanga  wa biashara ya utumwa hususan ile ya kuvuka bahari ya Atlantiki.

Sauti -
2'4"

Evros huko hali si shwari kwa wajawazito wakimbizi

Umoja wa Mataifa umeisihi Ugiriki iboreshe mazingira na kasi ya mapokezi ya wasaka hifadhi kwenye mkoa wa Evros ambako wakimbizi wanazidi kumiminika wakipitia mpaka wa nchi hiyo na Uturuki.

 

Sauti -
1'31"

Mila zetu za umiliki wa ardhi ndio muarobaini wa mivutano- Jamii ya asili

Jukwaa la kudumu la watu wa asili la Umoja wa Mataifa linakunja jamvi leo Ijumaa huku washiriki wakiweka msisitizo suala la kujumuisha sheria za umiliki wa ardhi za kimila ili kuepuka mizozo ya umiliki wa ardhi za watu wa jamii hiyo.

 

Sauti -
1'37"

Tekinolojia ya habari na mawasiliano yafufua matumaini ya wakimbizi Ujerumani

Hatua ya kutoa mafunzo ya teknolojia ya habari na mawasiliano au TEKNOHAMA kwa wakimbizi kupitia shule ya ReDi nchini Ujerumani, imefufua matumaini ya mustakhbali wao  waliokuwa wameukatia tamaa.

Sauti -
2'8"

Bila ufadhili mpya roho mkononi kwa maelfu ya Warohingya huko Bangladesh

Juhudi za mashirika ya umoja wa Mataifa za kunusuru maisha ya maelfu ya Warohingya waliokimbilia Bangladesh dhidi ya msimu wa pepo kali na mvua za monsoon zinazotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao , zitagonga mwamba endapo hakutapatika ufadhili mpya haraka. 

Sauti -
1'37"