Habari kwa Ujumla

Kweli nyumbani ni nyumbani: UNHCR

Wahenga walinena msahau kwao mtumwa, na nyumbani ni nyumbani hata iweje. Kauli hiyo si msemo tena bali ni hali halisi kwa maelfu ya wakimbizi wa Kisomali walioamua kuchukua hatua ya kurejea nyumbani baada ya kuishi kwa miaka mingi kwenye makambi ya wakimbizi ya Dadaab na Kakuma nchini Kenya.

Sauti -

MONUSCO yajenga uwezo polisi kuelekea uchaguzi mkuu DRC

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC,

Sauti -

Dola bilioni 1.7 zahitajika kusaidia wananchi wa Sudan Kusini

Mzozo nchini Sudan Kusini ukiingia mwaka wa nne, zaidi ya dola bilioni 1.7 zahitajika ili kukidhi mahitaji ya kibinadamu kwa nchini humo kwa mwaka 2018.

Sauti -

Taka za kielektroniki zasalia kwenye makabati majumbani- Ripoti

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imebaini ongezeko kubwa la taka za kielektroniki ulimwenguni.

Taka hizo ni pamoja na betri chakavu, plagi za umeme, majokofu, simu za kiganjani na kompyuta ambazo kiwango chake mwaka 2016 kilifikia tani za ujazo milioni 44.7.

Sauti -

Ukimpa mwanamke fursa, jamii itanufaika

Kuna usemi wa kwamba ukimuelimisha mwanamke umeielimisha jamii na ukielimisha  jamii basi utakua umeokoa  kizazi cha baadaye. Huu usemi  hauna maana ya upendeleo bali  ni ukweli kwamba ukimpa mwanamke fursa basi  jamii itanufaika zaidi.

Sauti -

Fedha sio tatizo kasi ya hatua zetu ndio tatizo : Guterres

Viongozi wa dunia leo wamekusanyika mjini Paris Ufaransa wakijaribu kusaka fedha zaidi ili kuusukuma uchumi wa dunia kuwa unaojali mazingira ikiwa ni miaka miwli kamili tangu kutiwa saini kwa mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tambia nchi kuepuka zahma kubwa zaidi ya ongezeko la joto duniani.

Sauti -

Madhila dhidi ya raia yaongezeka mzozoni Ukraine; UM

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa leo inasema madhila dhidi ya raia katika mzozo wa kivita nchini Ukraine huenda yakaongezeka zaidi, kufuatia kuibika upya kwa mapigano.

Sauti -

Watoto wapatao 400,000 wakabiliwa na utapiamlo kasai DRC: UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF,  limesema zaidi ya watoto 400,000 wenye umri wa chini ya miaka mitano huko  eneo la Kasai

Sauti -

Kampeni ya chanjo kwa watoto wa Rohingya yaanza :UNICEF/WHO

Serikali ya Bangladeshi kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, shirika la afya duniani

Sauti -

Kuwekeza kwenye Malaria ni hatua chanya- Dkt. Winnie

Uwekezaji katika kukabiliana na Malaria, ni uwekezaji ambao utasaidia siyo tu kutokomeza umaskini bali pia kuchochea maendeleo kwa ngazi ya jamii na taifa kwa ujumla.

Sauti -