Habari kwa Ujumla

ICTR yahitimisha kazi leo, Baraza la Usalama latoa pongezi

Wanachama wa Baraza la Usalama wamepongeza kazi zilizofanyika na mahakama ya kimataifa kuhusu mauaji ya kimbari Rwanda ICTR ambayo inahitimisha kazi zake leo.

Sauti -

Mukhtasari wa Matukio ya Mwaka 2015 Umoja wa Mataifa

Leo ikiwa ni Siku ya Mwisho ya Mwaka 2015, tunakuletea muhtasari wa matukio muhimu yaliyoangaziwa katika Umoja wa Mataifa mwaka huu.

Sauti -

Hali ya njaa yazidi kuwa mbaya Taiz Yemen: WFP

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP limeelezea leo wasiwasi wake kuhusu kuzorota kwa hali ya kibinadamu mjini Taiz nchini Yemen ambapo watu hukumbwa na njaa huku WFP ikishindwa kuwapelekea chakula.

Sauti -

Uzinduzi wa utekelezaji rasmi wa SDG's kuanza Januari Mosi: Ban

Siku ya mwaka mpya Januari Mosi inaashiria uzinduzi rasmi wa ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 (SDG's) iliyopitishwa na viongozi wa dunia Septemba mwaka jana kwenye Umoja wa Mataifa.

Sauti -

UNHCR yapambana na kipindupindu kwenye kambi ya Dadaab Kenya:

Wahudumu wa afya kwenye kambi kubwa kabisa ya wakimbizi duniani ya Dadaab Kenya, wanajitahidi kupambana na mlipuko wa kipindupindu ambao tayari umeshakatili maisha ya watu 10 na wengine takriban 1000 wameambukizwa tangu ulipozuka mwezi uliopita ukihusishwa na mvua kubwa za El Niño.

Sauti -

Ban ampongeza waziri mkuu wa Iraq kwa vita dhidi ya ISIL

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon leo amempigia simu waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abadi, na kumpongeza kwa mafanikio ya vikosi vya usalama vya Iraq kwa vita dhidi ya kundi la kigaidi la ISIL.

Sauti -

Rais wa Burundi apinga vikosi vya AU kuingia nchini mwake:

Rais wa Burundi ametupilia mbali mpngo wa Muungano wa Afrika wa kutuma vikosi vya walindamamani nchini mwake. Kiongozi amesema vikosi ikiwa vitaingia Burundi bila idhani ya serikali, vitachukulia kuwa bi majeshi ya uvamizi na serikali yake iko tayari kupambana nao.

Sauti -

Zaidi ya wakimbizi na wahamiaji milioni 1 wamewasili Ulaya 2015 kupitia bahari:UNHCR

Zaidi ya wakimbizi na wahamiaji milioni moja wamekimbilia Ulaya mwaka huu kwa njia ya bahari limesema shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi

Sauti -

Uzinduzi rasmi wa SDG’s kuanza Januari Mosi: Ban

Siku ya mwaka mpya Januari Mosi inaashiria uzinduzi rasmi wa ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 (SDG’s) iliyopitishwa na viongozi wa dunia Septemba mwaka jana kwenye Umoja wa Mataifa.

Sauti -

Wadau wote lazima kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa Amani CAR:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito kwa wadau wote nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR kuhakikisha uchaguzi wa Rais na wabunge unaofanyika leo unakuwa wa Amani na utulivu.

Sauti -