Habari kwa Ujumla

Ban awateua Kufour na Stolternberg kumsaidia masuala ya mabadiliko ya tabianchi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametangaza kuwateuwa wajumbe wawili ambao watawajibika katika eneo la mabadiliko ya tabia nchi. Walioteuliwa ni rais mstaafu wa Ghana John Kufuor na waziri mkuu wa zamani wa Norway Jens Stoltenberg.

Sauti -

UNMISS kuimarisha uwepo wake Unity na Jonglei; Ban ataka wanasiasa Sudan Kusini kuchukua hatua

Wakati hali ya amani inazidi kuzua sintofahamu huko Sudan Kusini, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Hilde Johnson ametoa taarifa akithibitisha mipango ya Umoja huo ya kuimarisha uwepo wa vikosi vyake kwenye maeneo ya Bor jimbo la jonglei na Pariang jimbo la Unity.

Sauti -

Ziarani Ufilipino, Ban ahuzunishwa na uharibifu wa kimbunga Haiyan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ambaye yupo ziarani nchini Ufilipino, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Benigno Simeon C. Aquino III wa Ufilipino, wakiangazia hasa juhudi za kibinadamu na kujikwamua kwa taifa hilo kufuatia janga la kimbunga Haiyan (Yolanda).

Sauti -

Ban aipongeza Madagascar kwa uchaguzi na kuwataka kulinda amani

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amewaongeza wananchi wa Madagascar, tume ya uchanguzi na watu wa serikali ya Malagasy  kwa ushiriki na mchango wao katika zoezi la uchaguzi wa rais na wabunge.

Sauti -

Umuhimu wa mshikamano baina ya binadamu waangaziwa nchini Kenya

Tarehe 20 mwezi Disemba ni siku ya kimataifa ya mshikamano iliyoidhinishwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa Disemba 22 mwaka 2005 katika azimo namba 60/ 209.  Ilibainishwa ndani ya azimio hilo kuwa mshikamano ni msingi na maadili ya kimataifa ya  kusisitiza mahusiano ya watu katika karne ya  21.

Sauti -

Ban asikitishwa na mauaji ya askari walinda amani Sudan Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon aamelaani vikali shambulio katika kituo cha ujumbe wa Umoja wa Matifa nchini Sudani Kusini

Sauti -

Ban awasili Ufilipino, kwenda Tacloban Jumamosi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon yuko nchini Ufilipino ambako anatarajiwa kuwa na mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo akiwemo Rais Benigno Aquino.

Sauti -

Madhila yawakumba raia wa Sudan Kusini kufuatia machafuko

Wakati hali ya sintofahamu ikiendelea kutajwa nchini Sudna Kusini , inaelezwa kuwa raia ndio wanaoathirika zaidi lakini watoto kwao hali ni tete kwani wanapatwa na magonjw aya milipuko huku wakikabiliana na chnagamoto za ukosefu wa huduma muhimukamamalazi bora, chakula na mengineyo.

Sauti -

Ofisi ya haki za binadamu yachukizwa na ukiukwaji wa haki Misri

Ofisi ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kitendo kilichofanyika huko Cairo, Misri cha kuvamia ofisi ya shirika la kiraia  linahusika na haki za binadamu na kukamatwa kwa watendaji sita kinatia hofu juu ya kuendelea kuongezeka kwa matukio hayo ya unyanyasaji dhidi ya vikundi hivyo nch

Sauti -

Serikali ya Syria na makundi ya upinzani yathibitisha kushiriki mkutano wa amani

Mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa nchi za Kiarabu kuhusu Syria, Lakhdar Brahimi amesema kuwa serikali ya Syria na makundi ya upinzani yamethibitisha kushiriki mkutano wa kimataifa mwezi ujao kuhusu amani nchini Syria, ambao utafaanza Januari 22 mwakani katika mji wa Uswisi w

Sauti -