Huko kwenye jimbo la Darfur, nchini Sudan watu wasiojulikana wameshambulia msafara wa kikosi cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika wa kulinda amani kwenye eneo hilo, UNAMID na kusababisha vifo vya walinda amani wawili, mmoja kutoka Senegal na mwingine kutoka Jordan.