Kamati ya Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa imeitaka serikali ya taifa la Djibouti kutekeleza kikamilifu sheria zinazolenga kuwalinda wanawake dhidi ya ukatili.
Wakala wa udhibiti matumizi ya nyuklia nchini Japan umetoa ripoti kuelezea hali ilivyo katika kinu cha Fukushima ambacho hivi karibuni kiliripotiwa kujitokeza kwa hitalafu iliyozusha wasiwasi wa kuibuka mionzi mikali.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa akifuatilia hali ilivyo huko Bangladesh na amesema ana wasiwasi mkubwa juu ya ongezeko la ghasia ambazo zimesababisha vifo vya watu kadhaa na wengi wamebaki majeruhi.
Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu kuhusu Syria Lakhdar Brahimi yuko nchini humo ambapo leo amekuwa na mazungumzo na Rais Bashar Al Assad.
Mnamo mwezi Oktoba, idadi kubwa ya wapiganaji wa kundi la waasi la M23 walijisalimisha kwa vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kuweka Utulivu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,
Watetezi wa haki za binadamu wanaofanya kazi kwa niaba ya jamii zinazoathiriwa na miradi mikubwa ya maendeleo kila mara hunyanyaswa na hata kupachikwa majina ya wapinga serikali au wapinga maendeleo pindi wanapokuwa wanatekeleza jukumu hilo.
Mwaka mmoja baada ya kimbunga Sandy kupiga maeneo ya Caribbean na pwani ya Mashariki ya Marekani, shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa limetaka kutosahauliwa kwa wahanga wa janga hilo hususan wale wa maeneo ya Caribbean.
Mtalaamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu uendelezaji wa demokrasia na usawa duniani Alfred de Zayas ameunga mkono wito unaotolewa wa kuwa na bunge la dunia, chombo ambacho amesema kitakuwa ni jibu la pengo la kidemokrasia linalojitokeza.
Hofu kubwa imetanda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kufuatia mapigano ya vikundi vyenye silaha na kuitaka serikali ya mpito kuingilia katika kuimarisha usalama huku hali ya misaada ya kibinadamu ikiendelea kuzorota nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC.