Habari kwa Ujumla

Mashauriano yafanyika Arusha katika jitihada za kutafuta amani ya kudumu Darfur, Sudan

Jimbo la Darfur nchini Sudan limekuwa na mzozo kwa miaka kumi sasa kati ya serikali na vikundi vya upinzani. Mzozo huo umesababisha mapigano ya mara kwa mara kwa misingi tofauti ikiwemo ile ya kikabila, kiuchumi na kisiasa.

Sauti -

Serbia na Kosovo zapiga hatia katika kuboresha uhusiano

Viongozi kutoka mataifa ya Serbia na Kosovo wamepiga hatua  ambapo makubaliano ya kihistoria yameafikiwa kwenye jitihada za kuboresha uhusiano kwa mujibu wa afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa nchini Kosovo .

Sauti -

ASIA-PACIFIC iko mbioni kuwapa ajira kwa watu wa kipato cha wastani: ILO

Shirika la kazi duniani ILO limesema ukuaji imara wa uchumi katika kanda ya Asia-Pacific kwa miongo miwili iliyopita kumesaidia kuwatoa ma

Sauti -

Rais wa baraza kuu asisitiza haja ya mageuzi UM

Wakati Baraza  kuu la Umoja wa Mataifa likikutana kutathmini kile kinachoonekana juhudi za mabadiliko ya utendaji kazi, rais wa baraza hilo amezitolea mwito nchi wanachama kuhakikisha kuwa zinapigania mageuzi yanayomulika karne 21 ambayo ni utendaji wa pamoja .

Sauti -

Wataalamu wa nchi zisizopitiwa na bahari kukutana Geneva

Wataalamu wa usafiri kutoka nchi zilizoendelea ambazo hazijafikiwa na mkondo wa usafiri wa majini, wanatazamiwa kukutana Geneva kwa ajili ya kujadiliana namna ya ufanikishaji wa sera zitazoziwezesha nchi hizo kupata huduma ya usafiri wa bahari.

Sauti -

Mapigano mapya DRC, Baraza la usalama latoa kauli

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wameshutumu kuzuka upya kwa mashambulio huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia yaCongo, DRC yaliyosababisha kifo cha mlinda amani kutokaTanzaniana majeruhi.

Sauti -

Familia za wale waliotoweka kwa lazima na mashirika yasiyokuwa ya serikali wahitaji kulindwa: UM

Mashirika ya umma na watu wa familia ambazo wapendwa wao hupotea wanahitaji kulindwa kutokana na vitisho huku pia wakihitaji kusaidiwa katika kazi zao.

Sauti -

Wawili wabainika kuwa na virusi vya homa ya Corona huko Qatar: WHO

Shirika la afya duniani, WHO limesema watu wawili wamethibitishwa kuwa na uambukizo wa kirusi cha homa yaCorona, MERS-CoV, nchiniQatar.

Sauti -

Ban akutana na kuzungumza na viongozi Uholanzi, amani duniani yaangaziwa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amekutana na kufanya mazungumzo na waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje wa Uholanzi katika tukio la maadhimisho ya miaka mia moja tangu ujenzi wa kasri la amani lililoko The Hague Uholanzi.

Sauti -

Askari mmoja wa kulinda amani wa UM auawa Goma, watatu wajeruhiwa

Umoja wa Mataifa umesema kuwa askari wake mmoja wa kulinda amani ameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa wakati wa operesheni ya kijeshi huko Goma Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Sauti -