Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amekaribisha makubaliano yaliyofikiwa jana kati ya seriakali ya Myanmar na shirika liitwalo Kachin Independence baada ya mkutano wao wa kwanza ndani ya nchi hiyo tangu kuzuka kwa mgogoro baina yao mwezi June mwaka 2011.
Nchini Ethiopia, wizara ya afya wiki ijayo inaanza kampeni ya dharura ya utoaji chanjo dhidi ya homa ya manjano baada ya kuthibitishwa kuwepo kwa wagonjwa Sita tarehe Saba mwezi wa Mei.
Kampeni hiyo inalenga kufikia zaidi ya watu Laki Tano maeneo ya kusini mwa nchi hiyo.
Wataalamu wa shirika la Umoja wa Mataifa la nguvu za Atomiki IAEA, wamehitimisha mafunzo ya siku nne yaliyowajengea uwezo wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali waliokutana Fukushima Japan.
Umuhimu wa usawa wa kijinsia na kumuwezesha mwanamke katika kuchagiza maendeleo barani Afrika itakuwa ajenda kuu kwenye mjadala wa ngazi ya juu utakaoendeshwa na mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleoo UNDP Bi Helen Clark kwenye mkutano wa kimataifa wa maendeleo ya Afrika utakao anza Ju
Kipengee kipya cha sheria kuhusu maji kimewasilishwa mbele ya kamati inayoongoza mazunguzo kuhusu sera nchini Georgia inayohusu usimamizi wa maji kwenye mkutano ulioandaliwa mjini Tbilisi tarehe 30 mwezi huu unaoungwa mkono na tume ya Umoja wa Mtaifa kuhusu uchumi barani ulaya UNECE.
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema imesikitishwa na hatua iliyochukuliwa na serikali ya Papua New Guinea ya kuelekea kurejea hukumu ya kifo. Taifa hilo linataka kurejea hukumu ya kifo baada ya kufanyia marekebisho sheria zake za uhalifu hatua iliyopitishwa na bunge Mai 28.
Dira na wajibu wetu ni kutokomeza ufukara kwa minajili ya kuweka maendeleo endelevu na ustawi wa kudumu kwa wote, hiyo ni kauli tangulizi ya ripoti ya jopo la watu mashuhuri lililoundwa kutoa mapendekezo ya ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015. Jopo hilo la watu 27 likiongozwa na Rais
Hatimaye jopo la watu mashuhuri lililoundwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kuandaa mapendekezo ya ajenda ya maendeleo baada ya ukomo wa malengo ya maendeleo ya milenia mwaka 2015, leo limewasilisha ripoti hiyo mjini New York ambapo pamoja na mambo mengine limetambua amani, haki za
Kuongezeka kwa viwavi au samaki wa baharini ni moja ya sababu kuu ya kupungua kwa samaki wengine hali ambayo imeshuhudiwa kwenye bahari ya Mediterranean na ile ya Black sea kwa mujibu wa ripoti ya shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa.