Habari kwa Ujumla

UM waendesha shabaya ya kuwasaidia waathirika wa Philippines

Umoja wa Mataifa unaendesha harakati za kukusanya kiasi cha dola za kimarekani milioni 28.6 kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa dhoruba la Kitropi lililowakumba wananchi walioko Kusini mwa Philipine.

Sauti -

Baraza la Usalama larefusha muda wa kusalia vikosi vya kulinda amani Abyei

Baraza la Usalama limerefusha muda kwa vikisi vya kulinda amani katika jimbo la Abyei ambalo linagambaniwa kati ya Sudan Kusini na Sudan kwa muda wa miezi mitano zaidi na kuzitolewa mwito pande hizo zinazozozana kuweka shabaya ya pamoja ili kutanzua mkwamo huo kwa wakati muafaka.

Sauti -

Sakata ya uundwaji wa katiba mpya inaendelea Tanzania

Suala la kuwa na katiba mpya si jipya hasa ukizingatia nchi nyingi duniani zinafanya mabadiliko na kujitahidi kwenda sambamba na hali halisi ikiwemo utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kama ya kutimiza haki za binadamu, kuwapa watu uhru wa kujieleza, kukuksanyika, kuupata elimu

Sauti -

Serikali ya Syria lazima isitishe mauaji ya watu:UM

Serikali ya Syria lazima izingatie makubaliano iliyotiwa saini na muungano wa nchi za Kiarabu Arab League wa kukomesha mauji ya watu.

Sauti -

Muda wa vikosi vya kulinda amani Golan waongezwa

Baraza la usalama limekubaliana kwa kauli moja kurefusha mamlaka ya Umoja wa Mataifa katika milima ya Golan ili kufanikisha mpango wa amani baina ya Israel na Syria.

Sauti -

Kiwango cha uchumi Amerika Kusini kushuka 2012

Hali ya ukuaji uchumi katika eneo la Latin Amerika na Carebbean inatazamiwa kushuka mwaka ujao kutokana na hali ya mkwamo wa uchumi wa dunia inayoshuhudiwa katika masoko kadhaa.

Sauti -

Baraza la usalama laongeza muda wa ofisi yake CAR

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa kuhudumu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kudumisha amani kwenye Jamhuri ya Afrika ya kati kwa mwaka mmoja zaidi kwa lengo la kuhakikisha kuwepo kwa mpangilio kwa kazi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini humo.

Sauti -

UNESCO yaelezea wasi wasi wa kuharibiwa kwa kituo ya kitamaduni mjini Cairo

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa lililotwikwa jukumu la kulinda utamaduni duniani limeelezea wasi wasi wake kutokana na kuripotiwa kwa ghasia kwenye mji mkuu wa Misri Cairo na kusababisha vifo vya watu 10 mwishoni mwa Juma na kuharibiwa kwa kituo cha kihistoria.

Sauti -

Ufadhili kutoka UM kuwasaidia wakulima nchini Lesotho

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na kuboresha maisha ya watu maskini wanaoishi vijijini linatoa dola milioni 10 ili kuwasaidia wakulima wadogo nchini Lesotho kuboreshaa kilimo.

Sauti -

Baraza la Usalama la UM laongeza muda wa ujumbe wa kisiasa nchini Burundi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa kuhudumu wa ujumbe wa kisiasa nchini Burundi likisisitiza kuwa nchi hiyo ni lazima ipige hatua katika kulinda haki za binadamu, kupigana na ufisadi, kufanyia mabadiliko sekta yake ya ulinzi na kuinua maendeleo ya uchumi.

Sauti -