Habari kwa Ujumla

UM wazindua muongo wa viumbe ili kuzuia kutoweka kwa familia za viumbe

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki–moon ametaka kuwe na urafiki kati ya ubinadamu na viumbe vingine kama moja ya njia ya kulinda manufaa yake kwa vizazi vijavyo.

Sauti -

Ban aitilia shime serikali ya Sri Lanka kukamilisha ahadi zake

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa anamatumaini makubwa kuwa serikali ya Sri Lank itatilia uzito na kutekeleza kwa vitendo ahadi zake ili kulifufua upya taifa hilo ambalo limepitia kwenye vipindi virefu vya vita vya kiraia.

Sauti -

UM kutoa chanjo ya polia kwa watoto wa Sudan Kusini

Mamia ya watoto nchini Sudan Kusini wapo katika mpango wa Umoja wa Mataifa wa utoaji chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo polio.

Sauti -

Wajasiliamali wa Kiafrika wapata tuzo ya UM

Kampuni moja nchini Gambia ambayo imefanikiwa kuleta teknolojia ya aina yake na nyingine nchini Kenya ambayo inamilikiwa na wanawake wanaotengeneza mafuta yanayoweza kuistamilisha ngozi ni miongoni mwa kampuni zilizoshinda tuzo la Umoja wa Mataifa kutokana na mchango wake wa kusaidia maendeleo en

Sauti -

Ocampo asisitiza haja ya kukamatwa kwa rais wa Sudan

Mwendesha mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu dhidi ya binadamu ICC amerejelea tena mwito wa kukamatwa na kufikishwa kwenye mahak

Sauti -

DR Congo na Burundi wajitahidi kupunguza maambukizi ya HIV

Wakati Ulimwenngu unaadhimisha siku ya kimataifa ya ukimwi, mapema mwezi huu nchi mbalimbali zinajitahidi kukimbizana na wakati ili kuhakikisha moja ya magonjwa sugu yanayoisumbua dunia katika karne hii ya 21, ukimwi, unadhibitiwa na hivyo kukaribia kutimiza lengo namba 6 la milenia ambalo ni kup

Sauti -

Baraza la Usalama larefusha muda kwa jopo la wataalamu wanafuatilia vikwazo kwa Liberia

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limerefusha muda kwa jopo la wataalamu linalofuatilia utekelezwaji wa vikwazo vilivyowekewa kwa Liberia, likiweka zingatio jipya juu ya uwezekano wa kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Sauti -

Mwendesha mashtaka juu ya kesi ya mauwaji ya waziri mkuu wa Lebanon Hariri asema atapumzika baada ya muhula wake kuisha

Mwendesha mashtaka katika mahakama iliyoundwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kufuatilia mauwaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri ameelezea nia yake ya kutoendelea kwenye wadhifa huo pale muda wake utakapokoma.

Sauti -

Mahakama ya ICTR yampunguzia kifungo afisa mmoja wa zamani

Mahakama ya Umoja wa Mataifa kuhusu uhalifu wa kivita iliyobainiwa baada ya kutokea mauaji ya halaiki nchini Rwanda ICTR imepunguza kifungo cha afisa mmoja wa zamani aliyehukumiwa mwaka uliopita kwa kuhusika kwenye mauaji ya halaiki ambapo maelfu ya watutsi waliuawa.

Sauti -

Afisi ya UM ya kuweka amani Jamhuri ya Afrika ya Kati yaomba usaidizi wa kifedha

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kuweka amani kwenye Jamhuri ya Afrika ya kati ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba mazungumzo kati ya serikali na makundi ya upinzani yanazaa matunda lakini ameonya kwamba ukosefu wa fedha huenda ukahujumu jitihada za kuwapokonya

Sauti -