Habari kwa Ujumla

Kumalizika kuondoka kwa vikosi vya Marekani Iraq kutaharakisha ujenzi imara wa taifa hilo:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa hatua ya kuondoka kwa vikosi vya Marekani nchini Iraq ni sawa na kusema kufunguliwa kwa ukurasa mpya katika historia ya nchi hiyo, ukurasa ambao unaleta enzi mpya.

Sauti -

Mtaalamu wa UM aitaka Canada kuzingatia ustawi wa jamii ya Attawapiskat ambao ni asili ya nchi hiyo

Mtaalamu huru anayefungamana na Umoja wa Mataifa katika eneo la haki za binadamu, ameitolea mwito Canada kuchukua hatua za haraka kuboresha hali ya ustawi wa baadhi ya wananchi wake ambao wanaendelea kuishi maisha ya taabu na dhiki huku wakikosa baadhi ya huduma muhimu ikiwemo maji.

Sauti -

Mabalozi wa Umoja wa Ulaya waitaka Israel kusitisha mpango wa ujenzi wa makazi ya walowezi

Wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya ambao wanaziwakilisha nchi zao kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wameitaka Israel kusitisha mara moja mpango wake wa ujenzi wa makazi ya walowezi katika mipaka ya Palestina ikiwemo pia eneo la Jerusalemu Mashariki.

Sauti -

Matumizi ya mmea wa Khat kama dawa ya kulevya wazua matatizo ya kiafya nchini Djibouti

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa matumizi ya mmea ujulikanao kama Khat limekuwa tatizo kubwa nchini Djibouti.

Sauti -

UM waitaka Syria kutekeleza mpango uliobuniwa Arab League

Umoja wa Mataifa umeendelea kuibana Syria kutekeleza mpango uliopendekezwa na Umoja wa nchi za kiarabu Arab League ili kutanzua mzozo unaofukuta sasa ambao umbao unatishia ustawi wa taifa hilo na wananchi wake.

Sauti -

UM waelezea shabaya yake ya kuendelea kuipiga jeki Aghanistan kukamilisha kipindi cha mpito

Umoja wa Mataifa imeihakikishia Afghanistan kuhusu vikosi vya kulinda amani kuendelea kufanya kazi huku pia ukielezea mashirikiano yake kwa taifa hilo kuwa yasiyoyumba wala kutetereka.

Sauti -

UNICEF yakaribisha hatua ya Israel kuwaachilia wafungwa watoto wa Palestina

Umoja wa Mataifa umekaribisha kuachiliwa huru kwa watoto 55 wa Kipalestina waliokuwa wakishikiliwa na Israel ikiwa sehemu ya mpango kwa pande hizo mbili kubadilishana wafungwa mpango ulioasisiwa miezi miwili iliyopita.

Sauti -

Mahakama ya UM yashikilia msimamo wa kupeleka kesi ya mchungaji Rwanda

Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayosikiliza kesi za mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 imetupilia mbali rufaa ya mchungaji wa zamani anayeshutumiwa kuchochea mashambulizi dhidi ya raia wa Kitutsi, na kusisitiza msimamo wake wa kupeleka kesi ya mchungaji huyo kuhukumiwa kwenye mahakama ya mf

Sauti -

Ban aelezea huzuni yake kufuatia kifo cha kiongozi wa DPRK

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea huruma yake leo kwa mamilioni ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea DPRK wanaoomboleza kifo cha kiongozi wao Kim Jong-il aliyefariki dunia Jumamosi.

Sauti -

Pillay alaani matumizi ya nguvu kwa waandamanaji Misri

Kamishna wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Navi Pillay amelaani vikali hatua ya vikosi vya kijeshi kuyaandama na kuyasambaratisha maandamano ya amani yaliyowakusanyisha mamia ya wananchi walipanga kuelekea kwenye uwanja wa Tahrir mjini Cairo kupinga mwenendo wa utawala wa kijeshi.

Sauti -