Karibu miaka miwili baada ya tetemeko kubwa la ardhi kuikumba Haiti na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200,000 taifa hilo linaonyesha dalili za kusimama tena. Hii ni kulingana na afisa wa Umoja wa Mataifa ambaye anasema kwamba jitihada za ujenzi mpya zinapaswa kupewa kipaumbele.