Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali tukio la kushambuliwa waandamanaji wa Syria iliyosababisha watu kadhaa kupoteza maisha na ameitaka serikali nchini humo kuzuia matumizi ya nguvu kudhibiti maandamano hayo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa hisia zake kufuatia ghasia zinazoshuhudiwa kusini mwa Israel na kwenye ukanda wa Gaza ambapo watu kadha wameuawa.
Kumeripotiwa mafanikio kwenye mazungumzo ya siku mbili kati ya viongozi wa Cypriot nchini Ugiriki na Uturuki pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.
Kundi la wataalamu wa mambo limetoa mwito likizitaka serikali duniani kuongeza mafungu ya kipato na kuboresha hali ya ustawi wa kijamii ili hatimaye kufadhilia amani na usalama pamoja na ukuzaji uchumi.
Jamii ya kimataifa imehimizwa kuweka zingatio la pamoja kwa kushagihisha mifumo yake ili hatimaye iweze kufaulu kukabili tatizo la ajira linaloiandama dunia kwa sasa.
Utafiti mmoja unaonyesha kuwa iwapo kutowekwa zingatia la kuondoa ziada ya risasi inayowekwa kwenye nishati ya mafuta, ulimwengu unaweza kupiga hatua kubwa na kufanikiwa kuzikwepa gharama zizozo za lazima.