Mashirika ya kimataifaa yameanzisha kampeni maalumu kuelekea kwenye kelele cha maadhimisho ya kimataifa ya siku ya ugonjwa wa moyo ugonjwa ambao hupoteza maisha ya watu zaidi ya milioni 17 kila mwaka.
Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yaani NCD's kama saratani, kisukari, maradhi ya moyo na matatizo ya kupumua sasa yamekuwa changamoto kubwa kwa mataifa yanayoendelea.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameitaka serikali ya Guinea kuvizua vikosi vyake juu ya matumizi ya nguvu za kijeshi hasa wakati huu ambao wananchi kadhaa wamejitokeza bara barani kwa maandamano ya amani.
Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na madawa ya kulevya na uhalifu ameonya kuwa hakuna njia ya mkato ambayo dunia inaweza kushinda vita ya usambazwaji wa madawa ya kulevya pasipo kuwepo kwa mashirikiano ya pamoja.
Zaidi ya familia 125,000 ambazo zinaishi maisha ya pangu pakavu nchini Rwanda, zitapatiwa misaada ya fedha kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao za kilimo.
Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia amewashauri raia wa nchi hiyo kuwa watulivu na kupiga kura kwa amani wakati Liberia inapojiandaa kwa uchaguzi wa Urais na wa Ubunge.
Taifa la Sudan Kusini lililozaliwa hivi karibuni hatimaye limekuwa miongoni mwa mataifa 34 yaliyopewa ufadhili wa fedha na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kutekeleza miradi yenye shabaha ya kutokomeza vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake.
Raia kadhaa wa Ghana na Nicaragua ambao wanaishi katika hali ngumu vijijini wanatazamia kupigwa jeki ili kuwasukuma mbele kiuchumi kufuatia mpango wa Umoja wa Mataifa wa ukuzaji uchumi unaotazamiwa kutekekezwa kwenye maeneo hayo.
Mkuu wa masuala ya kisiasa kwenye Umoja wa Mataifa amesema kuwa utawala wa Palestina una uwezo wa kuwa taifa. Bwana Lynn Pascoe amesema haya alipohutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali kwenye eneo la mashariki ya kati.