Habari kwa Ujumla

Ban kuanza ziara ya kutembelea mataifa manne

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anajiandaa kwa ziara ya kuyambelea mataifa manne itakayomchukua kuanzia Australia hadi katika visiwa na Solomon ambako anatazamiwa kutilia uzito masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.

Sauti -

Mgogoro wa kibiashara kati ya Kosovo na Serbia

Mvutano uliosababishwa na mgogoro wa kibiashara kati ya Kosovo na Serbia unaendelea. Kaimu mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Kosovo, Farid Zarif amelieleza Baraza la Usalama kwenye  mkutano hii leo.

Sauti -

Wahusika wa mashambulio ya bomu Abuja lazima wapelekwe mbele ya sheria: Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa UM Bi Asha Rose Migiro amelaani vikali mashambulio yaliyolenga majengo ya Umoja wa Mataifa nchini Nigeria.

Sauti -

Idadi kubwa ya wasomali yawasili Yemen

Zaidi ya Wasomali 3700 wamewasili Yemen wakibebwa na mashua kupitia Ghuba ya Aden.

Sauti -

Wahisani ni muhimu sana kwa mamilioni ya watu duniani:UM

Ijumaa ya tarehe 19 Agosti Umoja wa Mataifa na dunia kwa ujumla waliungana kuadhimisha siku ya kimataifa ya wahisani watu ambao mchango wao, kujitolea kwao na juhudi zao zimeokoa na zinaendelea kuokoa mamilioni ya watu katika maeneo yenye matatizo ya vita, njaa, majanga ya asili na kadhalika.

Sauti -

ICC yakaribisha hatua ya Grenada kuwa mwanachama mpya wa mahakama hiyo

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imekaribisha hatua ya Grenada ambayo wiki hii imeridhia mkataba wa Roma unaotambua uwepo wa mahakama hiyo

Sauti -

UNESCO yalaani mauwaji ya mwandishi wa Pakistan

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya elimu, sayansi, na utamaduni ambalo pia linawajibika na utetezi wa uhuru wa vyombo vya habari

Sauti -

Tuzo la ulinzi wa amani la Umoja wa Mataifa

Afisa wa polisi wa Pakistan ambaye amekabiliana na changamoto kadhaa wakati akitekeleza majukumu yake ya kipolisi ametunikiwa tuzo la Umoja wa Mataifa juu ya utunzaji amani.

Sauti -

Mkakati wa matumizi ya maji ya ziwa Victoria wazinduliwa Rwanda

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na makazi UN HABITAT limezindua awamu ya pili huko Rwanda yenye shabaya ya kuijengea uwezo nchi za Afrika mashariki juu ya matumizi ya maji ya ziwa Victoria.

Sauti -

Ban aitaka Sudan Kusini kurejesha utulivu kwenye eneo kulikozuka mapigano ya kikabila

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa mwito kwa serikali ya Sudan Kusini kurejesha hali ya utulivu katika jimbo la Jonglei ambalo limeshuhudia watu zaidi ya 600 wakifariki dunia kufuatia machafuko ya kikabila yaliyozuka wiki iliyopita.

Sauti -