Nchini Malawi mradi wa kuboresha lishe kwa watoto unaotekelezwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa na mdau Muungano wa Ulaya, umeleta matumaini makubwa kwa wazazi ambao watoto wao awali walikumbwa na udumavu uliotia mashaka uhai wao. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
Leo katika neno la wiki ambapo ni fursa ya kujifunza lugha ya Kiswahili, tunapata ufafanuzi wa maana za neno"MCHAPO" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania , BAKITA .
Leo ni Ijumaa na tunakuletea mada kwa kina na tunaangazia maonesho ya sanaa ya uchoraji picha yaliyofanywa jijini Nairobi Kenya na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na madawa na uhalifu, UNODC.
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP limesema njaa ni tatizo mtambuka ambalo linachangia nchi nyingi kushindwa kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs.