Kabrasha la Sauti


31 Desemba 2018

Jarida letu la kufunga mwaka hii leo ni mkusanyiko wa matukio  ya mwaka ukiletwa kwako na Siraj Kalyango na Grace Kaneiya. Hata hivyo kuna muhtasari wa habari muhimu hivi leo ikiwemo uchaguzi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Sauti -
9'55"

Kombe la amasaza kiungo muhimu cha kuunganisha jamii Hoima Uganda

Michezo ni moja ya mbinu ambazo zinaweza kutumika katika jamii ili kuendeleza amani na uwiano katika jamii. Nchini Uganda kwa kutambua umuhimu wa michezo, wameanzisha kombe la Amasaza la eneo la ufalme wa Bunyoro.

Sauti -
3'24"

Neno la Wiki- Paraganyika

Hii leo katika Neno la wiki, mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi wa  Baraza la  Kiswahili la Taifa nchini Tanzania-BAKITA na  anafafanua neno 'Paraganyika'.

Sauti -
54"

Nilikuwa na hofu ugenini, lakini sera za Rwanda zimeniondoa uhofu- Mhamiaji

Mpango wa kujumuisha wakimbizi katika maendeleo ya kiuchumi kwenye mji mkuu wa Rwanda, Kigali, umechangia katika wakimbizi kuanzisha biashara ndogo ndogo ambazo zimebuni ajira kwa watu 2,600 nchini humo, ikiwemo biashara ya kuuza mitungi ya gesi inayomilikiwa na mkimbizi kutoka Burundi.

Sauti -
2'15"

Kubinywa kwa haki za waandamanaji Sudan kwasababisha wataalamu wa haki kupaza sauti

Hii leo mjini Geneva, Uswisi, wataalamu wa Umoja wa Mataifa wameeleza hofu yao kuhusu kuongezeka kwa vurugu na kuuawa kwa waandamanaji nchiniSudan ambao wamekuwa wakipinga ongezeko la bei ya bidhaa na uhaba wa mafuta na chakula. Arnold Kayanda na maelezo zaidi.

Sauti -
1'19"

Chonde chonde tuepushe watoto na madhila zaidi mwaka 2018- UNICEF

Mwaka 2018 ukifikia  ukingoni, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetoa tathmini ya hali ya watoto mwaka huu hususan kwenye

Sauti -
2'11"

28 Desemba 2018

Jaridani hii leo na Siraj Kalyango tunaanza na Sudan ambako  yaripotiwa maelfu ya watu wanaandamana kupinga ongezeko la bei za bidhaa sambamba na uhaba wa chakula na mafuta ya gari.

Sauti -
11'44"

Kampuni ya Kijerumani yatuzwa Uganda kwa uhifadhi wa mazingira

Umoja wa Mataifa unahimiza uhifadhi na ulinzi wa mazingira kama njia mojawapo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Sauti -
3'42"

Mwanamazingira asema ndoto zake kupinga matumizi ya plastiki sio za abunuwasi

Mwezi Juni mwaka huu wakati wa siku ya baharí duniani, iliyokuwa na kaulimbiu- kuzuia matumizi ya plastiki na kuhamasisha hatua za kuwa na baharí salama- Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa haikusita kuzungumza na James Wakibia, mwanaharakati wa mazingira kutoka  Kenya, ambaye kwa miaka sita s

Sauti -
2'

Profesa Assad asema kuwa kutotekeleza mapendekezo ya ripoti ni jambo la kusikitisha

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali nchini Tanzania, CAG Profesa Musa Assad amezungumzia kitendo cha baadhi  ya ripoti zinazoonyesha  ubadhirifu kutoshughulikiwa ipasavyo na Bunge la nchi hiyo. 

Sauti -
1'30"