Ripoti ya mwaka 2011 kuhusu uhamiaji duniani ilibainika kwamba bado suala la uhamiaji linakabiliwa na changamoto nyingi. Bado watu wengi wanaendeleana kuhama kutafuta maisha mazuri hasa kutoka bara la Afrika kwenda Ulaya.
Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linafanya hima ili kutoa makao kwa maelfu ya familia zilizohama makwao baada ya kutokea kwa dhoruba kali iliyoikumba Ufilipino tarehe 17 mwezi huu.
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ametaka kuwe na ushirikiano baina ya wanachama wa Umoja wa Mataifa hasa kwenye masuala ya mabadiliko kwenye Umoja wa Mataifa , maendeleo na ustawi wa dunia.
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea kushangazwa kwake na uvamizi unaoendelea mjini Cairo nchini Misri kwenye mashirika kadhaa yasiyokuwa ya kiserikali mengi yakiwa ya haki za binadamu.
Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC imetuma msaada wa dharura wa madawa wakati kunapoendelea kushuhudiwa mapigano kwenye eneo la Middle Juba kusini mwa Somalia hasa maeneo ya Kismayo, Afmadow na Dhobley.
Shirika la afya duniani WHO limeelezea wasi wasi wake kuhusu utafiti unaofanywa na taasisi kadha kubaini mabadiliko ya hali ya hewa kwa virusi vya H5N1 likise
Mkuu wa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na kile cha Muungano wa Afrika UNAMID cha kulinda amani kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan amesema kuwa kuendelea kuwepo ukosefu wa usalama kwenye jimbo hilo kumewazuia walinda amani kufanya kazi yao.
Ugonjwa wa kipindupindu ambao ulitapakaa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa sasa unaripotiwa kuanza kutoweka lakini hata hivyo kunasalia visa vichache vya maambukizi ya ugonjwa huo.
Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na wakimbizi limekaribisha hatua ya serikali ya Georgea iliyoridhia mkataba wa kimataifa wenye nia ya kuwalinda na kuwatetea mamililoni ya watu walioko mtawanyikoni ambao hawana uhalisia wa nyumbani.