Sauti Mpya

Utapiamlo huigharimu Pakistan dola bilioni 7.6 kila mwaka: WFP

Madhara ya utapiamlo  ikiwa ni pamoja na gharama za juu za matibabu huigharimu Pakistan dola bilioni 7.6 sawa na asilimia tatu ya pato la taifa kila mwaka, imesema ripoti ya shirikal a mpango wa chakula duniani WFP.

Sauti -

Viwavijeshi waleta hofu kusini mwa Afrika

Uvamizi wa viwavijeshi kwenye mashamba kusini mwa Afrika kumezua sintofahamu siyo tu kwa wakulima bali pia wataalamu wa kilimo.

Sauti -

Vikwazo dhidi ya silaha za kemikali Syria vyagonga mwamba

Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililolenga kuweka vikwazo kufuatia matumizi ya silaha za kemikali nchin Syria limegonga mwamba baada ya Urusi na China kupinga kwa kutumia kura zao turufu.

Sauti -

Afrika itaendelea kuwa kipaumbele cha UM- Naibu Katibu Mkuu

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed leo ameapishwa rasmi na Katibu Mkuu wa umoja huo António Guterres ili kushika wadhifa huo baada ya kuteuliwa mwishoni mwa mwaka jana.

Sauti -

UM kutathimini haki za wazee Namibia

Mtaalamu wa haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa Rosa Kornfeld-Matte anatarajia kufanya ziara ya kwanza ya kikazi nchini Namibia kuanzia Machi pili hadi 13 mwaka huu kwa ajili ya kutathimini hali ya haki za binadamu kwa wazee nchini humo.

Sauti -

Tamasha la kibunifu kwa ajili ya SDG's kuanza kesho Bonn

Mkutano wa kwanza unaotumia michezo ya kidijitali kuchagiza ufumbuzi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDG's , unaanza kesho huko Bonn, Ujerumani ukitarajiwa kumalizika Ijumaa. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Sauti -

Ukosefu wa usalama wafurumusha watoa misaada 28 jimbo la Unity- OCHA

Nchini Sudan Kusini, wiki moja baada ya baadhi ya maeneo kutangazwa kukabiliwa na njaa, Umoja wa Mataifa umeomba pande kinzani kwenye mzozo nchini humo kuhakikisha usalama ili misaada ya kibinadamu iweze kuwafikia walengwa.

Sauti -

Watoto wavukao Mediteranea wakumbwa na ukatili wa kupindukia- UNICEF

Safari ya watoto wanaokimbia mizozo na mateso Afrika kwenda Ulaya kupitia bahari ya Mediteranea imegubikwana mateso ikiwemo ukatili wa kingono na utumikishwaji, imesema ripoti mpya ya shirika la kuhudumia watoto duniani,

Sauti -

Kampuni ya Skylon Global ya Kenya kidedea tuzo ya 2017 ya SheTrades

Kampuni ya Skylon Global kutoka Kenya, imeibuka kidedea na kunyakua tuzo ya SheTrades ya changamoto ya uwekezaji kwa mwaka 2017.

Sauti -

Kama serikali haiwezi kutoa huduma ya maji basi isiwe jinai kuyatafuta:UM

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya binadamu ya maji na usafi ameelezea hofu yake kuhusu mswada wa sheria wa hivi karibuni mjini Lagos Nigeria unaoharamisha utafutaji wa maji kupitia mali asili.

Sauti -