Sauti Mpya

Wataalam wa Umoja wa Mataifa wasikitikia ghasia kuenea na kuwalenga raia Sudan Kusini

Washauri maalum wa Umoja wa Mataifa wameelezea hofu yao kuhusu kulengwa kwa raia katika mapigano  ambayo yameanza kufuata mkondo wa ghasia za kikabila nchini Sudan Kusini.

Sauti -

Hatuondoki Sudan Kusini licha ya changamoto za kiusalama: Bi. Johnson

Hatutaondoka Sudan Kusini,  tupo hapa na tutaendelea kujiimarisha kwa maslahi ya wananchi, ni kauli ya Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Hilde Johnson alipozungumza na waandishi wa habari mjini Juba, ikiwa ni zaidi ya wiki moja tangu mapigano ya wenyewe kwa

Sauti -

Baraza la usalama kukutana leo kujadili kuimarisha UNMISS

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Hilde Johnson, leo amekuwa na mkutano na waandishi wa habari mjini Juba kuelezea hali halisi hivi sasa wakati ambapo raia Elfu 81 wamepoteza makazi yao tangu kuanza kwa mzozo huo zaidi ya wiki moja.

Sauti -

China yapiga hatua kuwaendeleza wanawake, lakini bado inakabiliwa na changamoto

Jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaohusika utokomezaji wa mifumo yote inayowakandamiza na kuwabagua wanawake limesifu namna Chinailivyopiga hatua kuendeleza ustawi wa wanawake, lakini hata hivyo limesema kuwa  bado kuna mengi yanapaswa kufanywa. Grace Kaneiya na taarifa kamili

Sauti -

Pillay ataka pande zinazopigana Sudan Kusini kujali maisha ya raia

Kamishna wa Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay amezitaka mamlaka zinazohusika katika mzozo wa Sudan Kusini kujiepusha na matumizi zaidi ya nguvu katika wakati ambapo taarifa zinasema kuwa mamia ya raia wameathiriwa zaidi baada ya mapigano hayo kuingia siku ya kumi.

Sauti -

Wataalamu waeleza kutoridhika na mbinu za uchunguzi dhidi ya watuhumiwa wa ugaidi

Wataalamu wawili huru wa masuala ya kibidamamu wa Umoja wa Mataifa hii leo wamekaribisha kuchapishwa kwa ripoti ambayo ni uchunguzi  unaohusu mateso na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu uliofanywa na uingereza dhidi ya watu wanaozuiliwa nchi za ng’ambo kwa minajili ya vita dhidi ya ugaidi.

Sauti -

Zaidi ya raia 81,000 Sudan Kusini wamekosa makazi-OCHA

Idadi ya watu waliopoteza makazi huko Sudani Kusini kutokana na machafuko yanayoendelea inakadiriwa kufikia jumla 81,000, lakini hata hivyo kuna uwezekano mkubwa wa idadi hiyo ikaongezeka.

Sauti -

UNHCR yachukua hatua za kusaidia wale waliohama makwao kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati

Huku makabiliano ya kijamii yakiendelea sehemu kadha za Jamhuri ya Afrika ya kati, shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR

Sauti -

WFP yasambazia msaada wa chakula raia Sudan Kusini

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linasambaza chakula kwa raia wa Sudan Kusini waliokimbia ghasia zinazoendelea nchini humo kwa zaidi ya wiki moja sasa.

Sauti -

Mapigano, mafuriko vyatatiza maisha ya raia Somalia

Wakati macho na masikio ya jumuiya ya kimataifa yakielekezwa nchini Sudan Kusini ambako kuna mapigano ya kikabila, nchi nyingine iliyoko pembe yaAfrika,Somalianayo inakabiliana na changamoto ya mapigano ya kikabila.

Sauti -