Kabrasha la Sauti


Takwimu mpya zadokeza idadi ya vifo nchini Syria kuwa zaidi ya Elfu 60

Kamishna Mkuu wa Tume ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema takwimu mpya zinadokeza idadi ya watu waliokufa nchini Syria kutokana na mapigano yanayoendelea ni zaidi ya Elfu 60.

Sauti -

Kemikali ya sumu au Aseniki iliyo kwenye maji yaweza kusababisha kansa

Ripoti mpya ya shirika la afya duniani, WHO, inasema uwepo wa kemikali ya sumu, aseniki katika maji ya kunywa na chakula kwa muda mrefu unaweza kusababisha sa

Sauti -

Uturuki yafungua milango kwa wakimbizi wa Syria kujiunga na vyuo vikuu.

Uturuki imeanzisha programu ambamo kwayo wakimbizi wa Syria nchini humo wanaweza kujiunga na vyuo vikuu vya umma bila malipo yoyote ya ada.

Sauti -

Ban amteua Jose Ramos-Horta kuwa mjumbe wake GUINEA –BISSAU

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemteua Rais wa zamani wa Timor-Letse José Ramos-Horta kuwa mwakilishi wake maalumu nchini Guinea Bissau.Kwa wadhifa huo pia, Ramos-Horta anakuwa Mkuu wa ofisi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini humo.

Sauti -

Kuimarisha amani nchini Somalia ni changamoto kubwa: Balozi Mahiga

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Balozi Augustine Mahiga amesema bado kuna changamoto kubwa kufanikisha amani ya kudumu nchini Somalia na kwamba ndoto ianyotarajiwa ni nchi hiyo kuwa salama, ustawi na amani ndani yake na kati yake na jirani zaike.

Sauti -

Mateka waliookolewa kurejeshwa nyumbani: UNPOS

 Umoja wa Mataifa kwa sasa unaongoza shughuli ya kuwarudisha makwao mateka waliookolewa hivi kutoka kwa maharamia wa kisomali baada ya miaka mitatu mikononi mwa maharamia hao.

Sauti -

Misaada zaidi yahitajika Afghanistan

Hali mbaya ya usalama na kudorora kwa hali ya kibinadamu huenda vikaikumba Afghanistan mwaka huu wa 2013, yamesema mashirika ya kutoa misaada. 

Sauti -

Walinda amani wawili wa Jordan waliokuwa wametekwa sasa huru: UNAMID

Walinda amani wawili wa Jordan waliotekwa wakati wakihudumu kwenye kikundi cha pamoja cha kulinda amani Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur, UNAMID wameachiwa huru baada ya kuwa matekani kwa siku 136.

Sauti -

MONUSCO yatoa majibu ya uchunguzi dhidi ya FDLR na uvumi mwingine huko Kivu Kaskazini

 Kundi la ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo MUNUSCO lililotumwa kubaini uvumi wa kuwasili kwa kundi la FDLR kutokaZambiakwenda mikoa ya Kivu ya Kaskazini wanasema kuwa uvumi huo si ukweli.

Sauti -