Bingwa wa kimataifa wa kandanda Yaya Touré ameteuliwa kama balozi mwema wa Shirika la mazingira duniani UNEP akiahidi kukabiliana na uwindaji haramu wa ndovu wa Afrika
Kamati ya Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa imeitaka serikali ya taifa la Djibouti kutekeleza kikamilifu sheria zinazolenga kuwalinda wanawake dhidi ya ukatili.
Wakala wa udhibiti matumizi ya nyuklia nchini Japan umetoa ripoti kuelezea hali ilivyo katika kinu cha Fukushima ambacho hivi karibuni kiliripotiwa kujitokeza kwa hitalafu iliyozusha wasiwasi wa kuibuka mionzi mikali.
Nchi zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara zinatazamiwa kuendelea kupata mafanikio ya kiuchumi katika msimu wa mwaka ujao 2014 tofauti na hali iliyoshuhudiwa katika kipindi cha mwaka 2013, limesema Shirika la fuko la fedha duniani IMF.
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limekutana na kusikiliza ripoti kuhusu majukumu ya mahakama ya kimataifa ya haki, ICJ na mahakama ya kimataifa ya uhalifu,
Zaidi ya wakimbizi Elfu Nane wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Gongo (DRC) wameingia wilaya ya Kisoro nchini Uganda tangu Jumatatu kufuatia mapigano katika Jimbo la Kivu ya Kaskazini. John Kibego wa redio washirika ya Spice FM, Uganda ametuma ripoti hii.