Kabrasha la Sauti


Sri Lanka inaelekea kwenye utawala wa kimabavu:Pillay

Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay leo amesema ingawa vita vimeishaSri Lanka, mateso bado yapo.

Sauti -

Ban apewa taarifa na mkuu wa upokonyaji silaha kuhusu Syria:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo Jumamosi Agosti 31 amekutana na afisa wa Umoja wa mataifa wa masuala ya upokonyaji silaha Bi. Angela Kane ambaye ndio amerejea kutokaDamascuskwenye uchunguzi wa silaha za kemikali na kupewa taarifa ya kinachoendelea hivi sasaSyria.

Sauti -

Mashauriano yafanyika Arusha katika jitihada za kutafuta amani ya kudumu Darfur, Sudan

Jimbo la Darfur nchini Sudan limekuwa na mzozo kwa miaka kumi sasa kati ya serikali na vikundi vya upinzani. Mzozo huo umesababisha mapigano ya mara kwa mara kwa misingi tofauti ikiwemo ile ya kikabila, kiuchumi na kisiasa.

Sauti -

Sintofahamu nchini Syria, Ban anashauriana na wajumbe wa kudumu wa Baraza la usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ambaye amekatiza ziara yake huko Austria na kurejea New York, Marekani kwa ajili  ya kushughulikia suala la Syria hivi sasa yuko katika mashauriano na nchi tano zenye ujumbe wa kudumu katika baraza la usalama la umoja huo. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Ma

Sauti -

AU yakamilisha warsha ya sheria za haki za binadamu kwa jeshi la Somalia:

Muungano wa Afrika AU leo umehitimisha mafunzo na warsha yenye lengo la kuboresha uelewa na utekelezaji wa sheria za kimataifa za haki za binadamu kwa maafisa wa jeshi la Somalia.

Sauti -

Serbia na Kosovo zapiga hatia katika kuboresha uhusiano

Viongozi kutoka mataifa ya Serbia na Kosovo wamepiga hatua  ambapo makubaliano ya kihistoria yameafikiwa kwenye jitihada za kuboresha uhusiano kwa mujibu wa afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa nchini Kosovo .

Sauti -

Wahamiaji wasio na vibali waliofukuzwa Tanzania kupatiwa misaada ya kibinadamu: IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limesema liko kwenye washirika wake huko Tanzania,Rwanda na Burundi kuona jinsi ya kuwapatia misaada ya kibinadamu maelfu ya wakimbizi wasio na vibali ambao wameamriwa kuondokaTanzania ndani ya wiki mbili.

Sauti -

WFP yaendelea na operesheni CAR licha ya usalama kuzorota

Huko Jamhuri ya Afrika ya Kati hali ya usalama inaendelea kuzorota kila uchwao lakini hilo halijakatisha tamaa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP katika kusambaza huduma za misaada.

Sauti -

ASIA-PACIFIC iko mbioni kuwapa ajira kwa watu wa kipato cha wastani: ILO

Shirika la kazi duniani ILO limesema ukuaji imara wa uchumi katika kanda ya Asia-Pacific kwa miongo miwili iliyopita kumesaidia kuwatoa ma

Sauti -