Sauti Mpya

IOM yasaidia wahanga wa mafuriko Zimbabwe

Mvua kubwa zilizoanza kunyesha katikati ya mwezi huu huko Zimbabwe zimesababisha mafuriko ambayo yameharibu miundombinu ya kijamii na kiuchumi ikiwemo barabara na shule.

Sauti -

Ban awapa hongera Wamisri kwa miaka miwili tangu mapinduzi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amepeleka salamu za heko kwa raia wa Misri, wakati wakiadhimisha miaka miwili tangu mapinduzi yaloing’oa serikali ya Hosni Mubarak mamlakani.  Bwana Ban ameelezea kujitolea kwa Umoja wa Mataifa kuwaunga mkono watu wa Misri na serikali yao kujenga mifu

Sauti -

Mwakilishi wa Ban huko CAR azungumzia azimio la Baraza la Usalama.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, Margaret Vogt amezungumza na waandishi wa habari kwa nchi ya video kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Bangui na kusifu azimio la Baraza la Usalama ambalo amesema linasisitiza umuhimu wa ofisi yake kutoa usaidizi wa ute

Sauti -

Baraza la Usalama laongeza muda wa ofisi yake huko CAR

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa ofisi yake ya ulinzi wa amani huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, BINUCA huku ikitaka serikali na vikundi vya upinzani kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano na mengineyo yenye lengo la kurejesha amani nchini humo.

Sauti -

Mali na Syria zatawala hotuba ya Ban huko Davos

Hali ya amani nchini Mali na Syria zinazidi kuzorota na hivyo tuchukue hatua haraka kwa pamoja, na huo ndio ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kwa viongozi mbali mbali wa dunia wanaohudhuria jukwaa la uchumi huko Davos Uswisi.

Sauti -

Ban akutana na Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amekutana na kufanya mashauriano na Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, wakati wa mkutano wa kimataifa kuhusu uchumi huko Davos, Uswisi.

Sauti -

IMF yatabiri ukuaji wa uchumi mwaka 2013

Shirika la fedha duniani IMF limesema kuwa kutakuwepo na ukuaji wa uchumi duniani mwaka huu wa 2013 wakati vizingiti kwenye masuala ya uchumi vinaporegea mwaka huu.

Sauti -

Ujerumani yatoa mchango wa Euro bilioni moja kwa mfuko wa Global Fund

Jamhuri ya Ujerumani imetoa mchango wa Euro bilioni moja kwa mfuko wa kimataifa wa kupiga vita UKIMWI, kifua kikuu na malaria, yaani Global Fund, ili kuwasaidia wahudumu wa afya kuendeleza juhudi za kuzuia na kutibu magonjwa haya hatari ya kuambukiza.

Sauti -

Ban afanya mashauriano na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amekutana na kufanya mashauriano na waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Bwana Ahmet Davutoğlu mjini Davos, Uswisi, ambako kongamano la kimataifa kuhusu uchumi linaendelea.

Sauti -

UNAIDS yazindua ukusanyaji maoni kupitia mtandao wa Intaneti

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na UKIMWI, UNAIDS, limefungua ukurasa huru wa mawasiliano ya kimtandao kwa shabaha ya kukusanya maoni toka pande zote za dunia, mawazo ambayo yatatumika kuratibu njia mpya za kukabiliana na tatizo la UKIMWI duniani.

Sauti -