Sauti Mpya

Wajawazito waona mwanga Somalia

Taifa la Somalia linazidi kuimarika kila uchwao baada ya kuundwa kwa serikali mwaka jana. Huduma za kijamii ikiwemo za kiafya zinazidi kuimarika.

Sauti -

Mafuriko Msumbiji yasababisha wengi kukosa makazi

Serikali ya Msumbiji kwa kushirikiana na mashirika ya misaada imeanzisha juhudi za kuwanusuru mamia ya wananchi ambao wameathiriwa kutokana na mafuriko makubwa yaliyokumba taifa hilo.

Sauti -

KASMO FM mkombozi wa wanawake Somalia

Kwa mara ya kwanza Somalia inapata kituo cha Radio kinachosimamiwa na kuendeshwa na wanawake, KASMO FM.

Sauti -

Katibu Mkuu wa UM asikitishwa na vifo vya vijana kwenye klabu: Brazil

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameeleza kuhuzunishwa kwake na vifo vya mamia ya vijana vilivyotokea kwenye klabu moja ya usiku kwenye mji wa Santa Maria, Rio Grande do Sul nchini Brazili.

Sauti -

Hali ya kibinadamu Syria yazidi kudorora

Umoja wa Mataifa unasema hali ya kibinadamu nchini Syria inazidi kudorora kila uchwao ambapo watu Milioni Nne wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Sauti -

Hakuna maendeleo endelevu kama kuna njaa: FAO

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa

Sauti -

Jumuiya ya kimataifa yaomba dola milioni 471 kwa ajili ya Afghanistan

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema kuwa watoto 165 walio na umri wa chini ya miaka mitano wanakufa kila siku huku mama mjamzito mmoja akifariki dunia kila baada ya saa mbili nchini Afhanistan.

Sauti -

Somalia, DRC, Madagascar, Zimbabwe zamulikwa huko Addis Ababa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekuwa na mazungumzo na viongozi wa Afrika ambapo wamefanya mashauriano kuhusu masuala kadhaa ikiwemo yua kiuchumi, kisiasa na kijamii. Taarifa zaidi na Alice Kariuki.

Sauti -

Bara la Afrika linasonga mbele: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameunga mkono maendeleo barani Afrika ikiwemo masuala ya utawala bora na haki za binadamu ambapo amesema mtazamo wake ni kwamba bara hilo linaibuka na kusonga mbele.

Sauti -

Ban asisitiza haja ya bara la Afrika kuwajibika kwa siku zake zijazo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema bara la Afrika lina uzoefu wa kulitosheleza kupata suluhu kwa changamoto zake, pamoja na kuchangia malengo ya kimataifa ya ukuaji unaowahusisha wote, haki ya kijamii na kulinda mazingira.

Sauti -