Sauti Mpya

Mamilioni ya watu Ulaya wanakata tamaa kufuatia mdororo wa kiuchumi: IFRC

Wakati bara la Ulaya likiwa bado linakumbwa na mdororo wa kiuchumi, Shirikisho la mashirika ya Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwekundu (IFRC) limeonya kuwa mamilioni ya watu ambao wameathiriwa na ukosefu wa ajira, ongezeko la umaskini, kupoteza makazi na hali ya sintofahamu kuhusu hatma yao huenda wak

Sauti -

Athari za kimbunga Msumbiji, mama ajifungulia juu ya paa: OCHA

Kimbunga Felling kimezidi kusababisha madhara huko Msumbiji wakati huu inapotolewa hadhari kuwa kinasonga kaskazini ambapo licha ya zaidi ya watu 48 kupoteza maisha na nyumba kuharibiwa za wakazi 250,000, mwanamke mmoja mjamzito amejikuta akijifungulia juu ya paa la nyumba.

Sauti -

Ongezeko la wanaouawa na askari wa Israel latia wasiwasi UM

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa  James W. Rawley ameelezea wasiwasi wake kutokana na kuongeza kwa watu wanaouawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel kwenye Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan.

Sauti -

Tumieni mkutano kuonyesha mnawajali raia wa Syria: Amos

Mkuu wa shirika la uratibu wa misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA, Valerie Amos amewasihi washiriki wa mkutao wa wahisani kwa ajili ya Syria huko Kuwait kutumia fursa ya mkutano huo kuonyesha kuwa wanajali na kushirikiana kuwasaidia wananchi wa Syria.

Sauti -

Ukata wa bajeti usikwamishe mchango kwa Syria: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumza katika mkutano wa wahisani kwa ajili ya Syria huko Kuwait na kusema kuwa mazingira magumu yanayokumba wasyria hayawezi kuachwa yaendelee licha ya kwamba serikali mbali mbali duniani zinakumbwa na ukata.

Sauti -

Utata uliopandikizwa kwenye tamko la Geneva juu ya Syria uondolewe: Brahimi

Mjumbe maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu kuhusu mgogoro wa Syria, Lakhdar Brahimi amelieza Baraza la Usalama kuwa hali ya Syria ni mbaya na kwamba anaona aibu vile ambavyo kila wakati amekuwa akirejea kauli hiyo bila hatua dhahiri kuchukuliwa.

Sauti -

UNICEF yaimarisha usaidizi wake kwa watoto huko CAR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linaimarisha operesheni zake huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ili kusaidia maelfu ya watoto wanaohitaji misaada ya dharura baada ya kujikuta katikati ya mzozo unaoendelea hivi sasa nchini humo.

Sauti -

IOM yasaidia wahanga wa mafuriko Zimbabwe

Mvua kubwa zilizoanza kunyesha katikati ya mwezi huu huko Zimbabwe zimesababisha mafuriko ambayo yameharibu miundombinu ya kijamii na kiuchumi ikiwemo barabara na shule.

Sauti -

Bado hatujaweza kufikia maeneo yote Syria: OCHA

Mkuu wa operesheni katika Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu,  OCHA, John Ging amesema hali  ya Syria bado inazidi kudorora kadri siku zinavyosonga na kwamba bado hawajapata kibali cha kuweza kuvuka eneo la mzozo na kuwafikia awle wote wanaohitaji misaada.

Sauti -

Marais na wanasoka wapaza sauti dhidi ya Malaria

Afrika Kusini, mwenyeji wa mwaka huu wa fainali za kombe la mataifa barani AFrika, AFCON. Wakati wachezaji wakipasha misuli yao kulinda nyavu zao, mbu nao wanavinjari kwa lengo la kuwamaliza nguvu..

Sauti -