Sauti Mpya

Hali ya usalama Syria inatia wasiwasi, pande husika zifanye mashauriano: Brahimi

Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na umoja wa nchi za kiarabu, kwenye mgogoro wa Syria Lakdhar Brahimi, amesema hali nchini Syria bado inatia wasiwasi na hivyo ametaka pande husika kwenye mgogoro huo kuchukua hatua madhubuti kwa ustawi wa raia wa Syria.

Sauti -

Ukeketaji wanawake ni kitisho kwa afya za wanawake: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumzia vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake ukiwemo ukeketwaji na kusema kuwa vitendo kama hivyo vinaweka hatarini afya za wanawake na wasichana wengi kote duniani.

Sauti -

Kinyang’anyiro cha nafasi ya Mkurugenzi Mkuu WTO chaendelea: Kenya yampendekeza Amina Mohammed

Idadi ya majina ya watu waliopendekezwa kuchukua wadhifa wa Ukurugenzi mkuu wa shirika la biashara duniani, WTO pindi Mkurugenzi Mkuu wa sasa Pascal Lamy atakapomaliza muda wake mwakani yamezidi kuongezeka baada ya Kenya kumteua Balozi Amina Mohammed kuwania nafasi hiyo.

Sauti -

Teknolojia ya anga za juu kutumiwa kupunguza athari za majanga: ESCAP

Nchi za Asia – Pasific zimeridhia mpango wa utekelezaji unaotumia teknolojia ya anga za juu kushughulikia majanga ya kiasili na hatimaye kufikia malengo ya maendeleo endelevu kwenye ukanda huo.

Sauti -

Mgao mkubwa zaidi wa mahitaji muhimu waendelea huko Goma, DRC: IOM

Mamia ya wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao wamekosa makwao kutokana na machafuko yanayojiri katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo wameanza kupokea misaada muhimu ikiwemo vifaa vya kujikimu huku wasambazaji wa huduma hizo wakikabiliana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Sauti -

Ulimwengu unaendelea kushuhudia dhuluma mbalimbali dhidi ya wanawake

Ulimwengu unaendelea kushuhudia dhuluma mbalimbali dhidi ya wanawake, ikiwemo ukatili, kwa madai eti ni utekelezaji wa mila na desturi za jamii husika.

Sauti -

Jeshi la Sudan ladaiwa kufanya mashambulizi ya anga, raia wakimbia: UNAMID

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika unaolinda amani kwenye jimbo la Darfur, nchini Sudan UNAMID, umeeleza wasiwasi wake juu ya ripoti za raia kukimbia makazi yao kutokana na mashambulio ya anga yanayodaiwa kufanywa na jeshi la Sudan na vikundi vyenye silaha huko Shangil Tobaya

Sauti -

UM wakaribisha hatua ya Senegal ya kumfungulia mashtaka rais wa zamani wa chad Habre

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imekaribisha hatua ya bunge la Senegal ya kupitisha sheria ya kubuniwa kwa sehemu ya mahakama itakayoendesha kesi dhidi ya rais wa zamani wa Chad Hissene Habre.

Sauti -

WFP kurejelea usambazaji wa chakula kwa watoto wanaotaabika nchini Swaziland

Shirika chakula la Umoja wa Mataifa WFP litarejelea shughuli za usambazaji wa chakula kwa vituo 1600 vya huduma nchini Swaziland baada ya shughuli hiyo kuvurugwa mapema mwaka huu kutokana na ukosefu wa ufadhili.

Sauti -

Wakazi wa Haiti waishio kambini bado wakumbwa na madhila makubwa: IOM

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la uhamiaji duniani, IOM pamoja na mashirika yake imeonyesha madhila ambayo bado yanawakumba wakazi wa Haiti kufuatia majanga ya mfululizo yaliyokumba nchi hiyo kuanzia mwaka 2010.

Sauti -