Sauti Mpya

Wengi wa walio na matatizo ya akili hawapati matibabu kwenye nchi zinazoendelea:WHO

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa thuluthi mbili ya watu walio na matatizo ya akili kwenye nchi zinazoendelea hawapati huduma za matibabu.

Sauti -

Ban aahidi kufanikisha kazi isiyowezekana

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amejitolea katika kufanikisha kile ambacho amekitaja kama kazi isiyowezekana.

Sauti -

Ban ampongeza Kiir kwa jitihada zake za kulinda raia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amefanya mazungumzo na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akimpongeza kwa kujitolea kwake katika kuwalinda raia na kwenye jitihada zake za kutafuta suluhu kwa mzozo unaondelea kati ya jamii ya Lou Nuer na Murle kwenye jimbo la Jonglei.

Sauti -

Afrika kuwa ajenda kuu kwa FAO

Mkuu mpya wa shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa

Sauti -

Umoja wa Mataifa kubadilika kuambatana na karne ya ishirini na moja:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa Umoja wa Mataifa unastahili kufuata mabadiliko ya karne ya ishirini na moja ili uweze kukabiliana vilivyo na changamoto za dunia.

Sauti -

UM wapiga hatua ya kukabiliana na Ukimwi kwa mwaka wa 2011

Mwaka 2011 umetajwa kama mwaka wa mabadiliko hasa kwenye vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi. Suala la ukimwi limekuwa likionekana kuwa changamoto kubwa lakini sayansi, mchango wa kisiasa na kujitolea kwa jamii vimesababisha kuwepo kwa mafanikio katika vita dhidi ya ukimwi.

Sauti -