Sauti Mpya

Matumizi ya kura ya veto yadhibitiwe

New Zealand imetaka mataifa matano yenye ujumbe wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yajidhibiti katika matumizi ya kura ya veto.Wito huo umetolewa siku ya Jumamosi na Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand Murray McCully wakati akihutubia mkutano wa 67 wa Baraza Kuu la Umoja wa

Sauti -

Sudan yaelelezea kujitolea kwake kusuluhisha mzozo na Sudan Kusini kwa njia ya amani

Serikali ya Sudan imesema itaendelea kutafuta suluhu kwa mzozo kati yake na Sudan Kusini kwa njia ya amani. Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, Ali Ahmed Karti katika hotuba yake kwenye kikao cha 67 cha mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.

Sauti -

Bara la Afrika ni lazima liwe na uakilishi kwenye Baraza la Usalama, wasema mawaziri kwenye mkutano wa Baraza Kuu

Mawaziri kutoka bara la Afrika wameuambia mkutano wa Baraza Kuu kwamba wanataka lipanuliwe Baraza la Usalama ili bara la Afrika lipate uakilishi wa kudumu kwenye baraza hilo.

Sauti -

Iceland kusaidia nishati asilia Afrika Mashariki

Serikali ya Iceland imesema inanzisha programu ya kuzalisha nishati asilia na salama itokanayo na joto la ardhini kwa manufaa ya mamilioni ya wakazi barani Afrika.

Sauti -

Ban akutana na rais Sein wa Myanmar

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amekutana na rais wa Myanmar Thein Sein Jumamosi asubuhi.Katika mkutano huo, viongozi hao wawili wamebadilishana mawazo kuhusu mabadiliko ya kisiasa nchini Myanmar, pamoja na maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na maridhiano ya kitaifa.

Sauti -

Waathiriwa wa ubakaji wa kuchochewa kisiasa Guinea-Conakry bado hawajapa haki: UM

Kuna haja ya dharura ya kuwasaidia manusura wa wa machafuko yalofanyika Guinea-Conakry na kuwachukulia hatua za kisheria waliotekeleza ubakaji na uhalifu mwingine.

Sauti -

Vijana wanafaa kuwa nguzo katika maendeleo ya Somalia: UNDP

Huku zaidi ya asilimia 70 ya idadi ya watu Somalia ikiwa ni vijana wenye umri chini ya miaka 30, kuwapa uwezo vijana itakuwa muhimu kwa ajili ya siku za baadaye za nchi hiyo, limesema Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP.

Sauti -

Tanzania yalitaka bara la Afrika kuungana katika kudai uanachama wa Baraza la Usalama la UM

Tanzania imetoa wito kwa bara la Afrika kuungana kuhusu suala la uakilishi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Sauti -

Gurudumu la mabadiliko Somalia halirudi tena nyuma: Balozi Mahiga

Nchi ya Somalia imepongezwa na viongozi kadha wa kadha, akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ban Ki-Moon, kutokana na jitihada ambazo imepiga kwenye mabadiliko ya kisiasa.

Sauti -

WHO yasisitiza umuhimu wa chanjo kwenye siku ya Kichaa cha Mbwa duniani

“Chanja mbwa, uokoe maisha” huu ni ujumbe kutoka Shirika la Afya Duniani ( WHO ), katika kuadhimisha siku ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa duniani, leo septemba

Sauti -