Sauti Mpya

Balozi Mahiga atoa wito Msaada Uongezwe Kuisaidia Somalia

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika maswala ya Somalia, Augustine Mahiga, ametowa wito kwa jamii ya kimataifa iongeze juhudi zake katika kulisaidia taifa hilo la pembeni mwa Afrika. Mahiga amesema haya wakati wa mkutano wa pili wa kimataifa kuihusu Somalia.

Sauti -

Mahitaji ya Kibinadamu Yaongezeka kwenye ghasia za Kivu ya Kaskazini, DRC

Watu 100,000 wamelazimika kutoroka makwao kufuatia ghasia za hivi karibuni katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini, mashariki mwa Congo na kupelekea Umoja wa Mataifa kutoa wito zifanywe juhudi bora zaidi za kulinda raia na msaada zaidi kwa walioathirika.

Sauti -

Mkuu wa UNHCR anasema kuna Ongezeko la Migogoro

Inakuwa ni vigumu kupata suluhu kwa watu walioko katika hali ya ukimbizi duniani amesema mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhdumia wakimbizi

Sauti -

Kamati ya UM yalaani Mauaji ya Watoto Syria

Kamati ya Umoja wa Mataifa ya haki za mtoto imelaani vikali mauaji ya watu 108 wakiwemo watoto 49 huko El Houleh Syria Ijumaa na Jumamosi iliyopita.

Sauti -

Kiongozi wa Sierra Leone ahaidi Uchaguzi Huru

Licha ya changamoto zinazoikabili Sierra Leone, nchi hiyo imepiga hatua kubwa tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka 10 iliyopita kwa mujibu wa mwakilishi wa Afrika ya Kusini kwenye Umoja wa Mataifa.

Sauti -

UM waitaka Tajikistan kuongeza fedha katika huduma ya Matatizo ya Akili

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya afya Anand Grover ameitaka serikali ya Tajikistan kuongeza fedha za matumizi ya afya ili kufikia kiwango cha kimataifa na kuanzisha haraka mfuko wa fadhili wa huduma za afya utakaohakikisha fursa ya huduma za afya kwa wote.

Sauti -

Idadi ya Vifo na Majeraha yapungua nchini Afghanistan mwaka huu:UM

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan umesema kuwa idadi ya watu waliouawa kwa kipindi cha miezi minne ya mwaka huu ilipungua kwa asilimia 21 ikilinganishwa na ya kipindi kama hicho mwaka uliopita nchini Afghanistan.

Sauti -

Ban akaribisha kundoka kwa vikosi vya Sudan Kusini kutoka eneo la Abyei

Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha kuondoka kabisa kwa vikosi vya Sudan Kusini kutoka eneo linalozozaniwa la Abyei.

Sauti -

Matumizi ya Silaha siyo Suluhu ya Kumaliza Tatizo Syria

Afisa mmoja kutoka Umoja wa Mataifa amesema kuwa kuendelea kushadidi kwa matumizi ya silaha katika maeneo yanayokabiliwa na mikwamo nchini Syria, hakuwezi kutoa suluhu badala yake ni kuangamiza eneo hilo.

Sauti -

UNHCR yahofia raia wa Syria walioko Kaskazini mwa Iraq

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, limeelezea wasiwasi wake kuhusu ongezeko la idadi ya raia wa Syria wanaokimb

Sauti -