Sauti Mpya

Tanzania yapiga hatua katika vita dhidi ya malaria

Tanzania imeanza kupata mafanikio kwenye juhudi za kukabiliana na ugonjwa wa malaria,ugonjwa ambao unatajwa kuwa miongoni mwa unaosababisha vifo vingi.

Sauti -

Wanawake zaidi wanatakiwa kwenye mabaraza ya maamuzi

Baraza la Usalama limepewa shime kuunga mkono juhudi zinazotaka kuongezeka kwa idadi ya wanawake kwenye mabaraza ya maamuzi

Sauti -

Ban aitaka Bahrain kuheshimu haki za msingi za binadamu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka mamlaka za Bahrain kujiweka kando na matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu na wakati huo huo amewatolea mwito viongozi wa taifa hilo kuwatendea haki raia inaoendelea kuwashikilia kwenye vizuizi.

Sauti -

Baraza la Usalama lalaani vikali mashambulizi kwa vikosi vya kulinda amani vilivyoko Darfur

Baraza la Usalama kwa kauli moja limelaani vikali matukio ya kushambuliwa kwa vikosi vya ulinzi wa amani katika eneo la magharibi wa jimbo la Darfur nchini Sudan , ambako maafisa wane walijeruhiwa na mmoja kati yake anasadikika kufariki dunia kutokana na majeraha makubwa.

Sauti -

Asia inahitaji nishati safi kukuza uchumi:ESCAP

Kuleta uwiano wa maendeleo endelevu na kiwango kikubwa cha ukuaji wa uchumi kunahitaji makubaliano ya nishati mpya kwa mataifa ya Asia na Pacific amesema afisa wa Umoja wa Mataifa anayehusika na mataifa hayo kwenye kongamano la watunga sera lililofanyika Jumatano.

Sauti -

Hukumu ya Charles Taylor kutolewa Alhamisi

Hukumu ya kesi dhidi ya Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor inatarajiwa kutolewa Alhamisi Aprili 26.

Sauti -

Nchi wanachama wanapunguza tofauti za jukumu la Shirika la UM la Biashara

Nchi wanachama bado hawajaafikiana kuhusu jukumu la shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo kwa miaka mine ijayo, lakini wanafanya juhudi kupunguza tofauti zao.

Sauti -

Masharti mapya kwa NGO's yanagandamiza haki za binadamu:Pillay

Kamishina Mkuu wa Haki za Binadam wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay Jumatano ameelezea hofu yake kuhusu hatua ya hivi karibuni katika baadhi ya nchi kuondoa uhuru wa mashirika yasiyo ya kiserikali yaani NGO’s na jumuiya zingine za kiraia kufanya shughuli zao kwa uhuru na inavyostahili.

Sauti -

Ushirikiano wa biashara wa Kusini-Kusini ni muhimu:UNCTAD

Mawaziri na maafisa kutoka pande zilioridhia maafikiano ya mfumo wa kimataifa wa kutoa kipaumbele katika masuala ya biashara miongoni mwa nchi zinazoendelea GSTP wamerejea kuonyesha nia yao ya kuyaleta matokeo ya Sao Palo katika utekelezaji kwa kusistiza mipango ya nchi kuridhia.

Sauti -

Mradi unaoongozwa na Global Fund wapunguza gharama za dawa za Malaria Afrika

Mradi unaoongozwa na Mfuko wa Kimataifa wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria yaani Global Fund kwa ajili ya kuzifanya dawa za kudhibiti Malaria kupatikana kwa gharama nafuu katika jamii za vijijini barani Afrika umeanza kupiga hatua kubwa.

Sauti -