Sauti Mpya

Stemp ya kuelimisha kuhusu Autism yatolewa na UM

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya matatizo ya afya ya akili au Autism hapo Aprili pili uongozi wa huduma za posta wa Umoja wa Mataifa umetoa aina 8 za stempu ili kuelimisha umma kuhusu matatizo hayo.

Sauti -

WFP yapeleka kwa ndege msaada wa chakula Chad

Shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limekamilisha kupeleka kwa ndege msaada wa haraka wa lishe kwa maelfu ya watoto walio katika hatari ya kupata utapiamlo nchini Chad, taifa ambalo limekumbwa na ukame.

Sauti -

Pillay kufanya ziara ya kwanza kabisa nchini Barbados

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay atafanya ziara rasmi nchini Barbados kwa mwaliko wa serikali kuanzia tarehe 3 hadi 5 mwezi Aprili mwaka huu.

Sauti -

Zaidi ya watu 100,000 wakimbia mapigano kaskazini magharibi mwa Pakistan

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limetoa usaidizi kwa maelfu ya familia nchini Pakistan ambazo zimekimbia map

Sauti -

Uchaguzi utakaoandaliwa nchini Myanmar utakuwa mtihani kwa taifa hilo:Quintana

Mjumbe maalum  wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Myanmar Tomas Ojea Quintana amesema kuwa uchaguzi mdogo unaotarajiwa kundaliwa tarehe moja mwezi ujao nchini Myanmar utakuwa jaribio kwa hatua zilizopigwa na serikali  katika masuala ya mabadiliko ambapo viti 48 vya bunge v

Sauti -

Raia wa Chad waliorejea nyumbani wanahitaji msaada:IOM

Uchunguzi wa IOM kwa wahamiaji kutoka Chad waliorejea kutoka Libya inasema kwamba wengine wanahitaji msaada wa dharura kuunganishwa na jamii zao.

Uchunguzi huo pia uligundua kuwa waliorejea nyumbani wamekumbana na changamoto zikiwemo za  kifedha za kujitafutia  na kwa familia zao.

Sauti -

Afisi ya haki za binadamu ya UM yahuzunishwa na kuuawa kwa msenge nchini Chile

Afisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea mshangao wake kutokana na kuuawa kwa mwanamme mmoja msenge nchini Chile.

Afisi hiyo sasa inatoa wito kwa serikali ya Chile kuweka sheria ambayo itapiga marufuku kutengwa kwa watu kuambatana na tabia zao za kimapenzi.

Sauti -

Ugonjwa wa Surua waua zaidi ya watoto 100 nchini Yemen

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa mkurupuko wa ugonjwa wa surua umewaua watoto 177 nchini Yemen huku wengine 40

Sauti -

LRA yafanya uvamizi zaidi kwenye Afrika ya kati

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa limepokea ripoti za uvamizi unaoendeshwa na kundi la Lord’s Re

Sauti -

Serikali ya Syria yatakiwa kusitisha ghasia mara moja

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na muungano wa nchi za kirabu  nchini Syria Kofi Annan amesema kuwa serikali ya Syria ni lazima iwe ya kwanza kutangaza usitishaji wa ghasia na iondoe wanajeshi wake kutoka sehemu waliko raia.

Sauti -