Kabrasha la Sauti


Mradi wa maji waleta nuru kambi ya Dadaab

Kambi ya Dadaab iliyoko Kaskazini Mashariki mwa Kenya inahifadhi wakimbizi kutoka Somalia. Kambi hii inaelezwa kuwa ni kubwa kuliko kambi zote za wakimbizi duniani ikiwa inahifadhi wakimbizi zaidi ya Laki Nne na Nusu. Uhaba wa maji umekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo.

Sauti -

Umoja wa Mataifa wapitisha azimio la kupiga vita ukeketaji wa wanawake

Makala yetu wiki hii ambayo pia ni ya mwisho kwa mwaka huu wa 2012 inaangazia Azimio la aina yake lililopitishwa na Umoja wa Mataifa la kupiga vita ukeketaji wa wanawake.

Sauti -

Azimio la UM kwa UNEP ni la kihistoria na linatoa fursa zaidi kwa wanachama wa UM: Steiner

Mwezi Disemba mwaka 2012 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio kuhusuu shirika lake linalohusika na mazingira, UNEP.

Sauti -

Kampuni ya sukari ya Mumias nchini Kenya na uhifadhi wa mazingira

Harakati za viwanda kujaribu kuhifadhi mazingira kwa kutumia mabaki ya malighafi za bidhaa zake kuzalisha bidhaa nyingine zinazidi kushika kasi, na viwanda kuwa mifano kwa viwanda vingine kama njia mojawapo ya kuhifadhi mazingira huku zikijiibulia huduma zingine.

Sauti -

Baraza la Usalama limechukua hatua madhubuti kulinda tembo: CITES

Mtendaji Mkuu wa Mkataba wa kimataifa wa udhibiti wa biashara ya viumbe vilivyo hatarini kutoweka, CITES, John Scanlon amesifu wito wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kutaka uchunguzi dhidi ya madai kuwa waasi wa kikundi cha LRA wanaua tembo na kuuza meno yao kimagendo.

Sauti -

Ulimwengu unaendelea kushuhudia dhuluma mbalimbali dhidi ya wanawake

Ulimwengu unaendelea kushuhudia dhuluma mbalimbali dhidi ya wanawake, ikiwemo ukatili, kwa madai eti ni utekelezaji wa mila na desturi za jamii husika.

Sauti -

Waasi Mali vunjeni uhusiano na vikundi vya kigaidi: Azimio Baraza la Usalama la UM

Kwa kutambua athari za mzozo wa mali kwa amani na usalama duniani, hii leo Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio ambalo pamoja na mambo mengine linataka waasi nchini humo kuvunja mara moja uhusiano na vikundi vya kigaidi ikiwemo Al-Qaida na kuthibitisha hatua hiy

Sauti -

UNAMID yapata kiongozi mpya: Ni Mohamed Ibn Chambas

Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika wamemtangaza Mohamed Ibn Chambas kuwa kiongozi mpya wa UNAMID ambao ni ujumbe wa pamoja wa pande mbili hizo wa kulinda amani kwenye jimbo la magharibi mwa Sudan, Darfur.

Sauti -

Usalama kambi ya Mugunga huko Goma si nzuri: Wanawake wapaza sauti zao

Umoja mataifa kupitia msimamizi Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani, Herve Ladsous umetangaza bayana kuwepo kwa sintofahamu ya hali ya usalama huko Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC.

Sauti -

UNECE yaidhinisha mkataba wa kukabiliana na uchafuzi wa hewa angani

Mkataba wa kimataifa wa matumizi ya vito vizito umepiga hatua baada ya kuungwa mkono na mataifa kadhaa kufuatia jitihada za majadiliano za miaka 3.

Sauti -