Sauti Mpya

Watu 10 wauawa kwenye mapigano katika eneo la Isiolo nchini Kenya

Takriban watu 10 wameripotiwa kuuawa kwenye eneo lililo kaskazini mwa Kenya la Isiolo kufuatia mapigano kati ya jamii za wafugaji zinazogombania malisho ambapo pia watu 2000 wamelazimika kuhama makwao kwa muda wa siku tatu zilizopita.

Sauti -

Mpango wa WFP kuwasaidia wakulima wa mahindi nchini Zimbabwe

Wakulima nchini Zimbabwe wamerejelea tena kilimo cha mahindi kutokana na mpango unaowasaidia kuuza mazao yao na kupata malipo yao wakati ufaao.

Sauti -

Ban ashutumu matumizi ya nguvu katika kutatua tofauti nchini Guinea Bissau

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameshutumu matumizi ya nguvu katika utatuzi wa mizozo nchini Guinea Bissau na kutaka kuheshimiwa kwa sheria kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi.

Sauti -

Kampuni ya Gucci yatoa dola milioni 1.15 kwa shirika la UNICEF

Kampuni ya kuuza bidhaa za kifahari ya Gucci imetangaza msaada wa dola milioni 1.15 kwa shirika ka kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF kwa

Sauti -

Juhudi za uokoaji zaendelea kwa waathiriwa wa dhoruba nchini Ufilipino

Oparesheni za kutoa misaada ya dharura ikiwemo makao, maji, chakula na usafiri kwa sasa zinaendelea kwenye kisiwa cha Mindanao nchini Ufilipino kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na dhoruba kwa jina Washi iliyosomba vijiji.

Sauti -

Ujumbe wa UM nchini Haiti watuma risala za rambi rambi kwa familia za waliokufa baharini

Mkuu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Haiti ametuma risala za rambirambi kwa rais wa nchi hiyo na kwa familia za watu 38 ambao walikufa baharini baada ya mashua walimokuwa kuzama juma lililopita mashariki mwa pwani ya Cuba.

Sauti -

UNHCR yaanza kuwasambazia wakimbizi wa Afghanistan mahitaji ya kumudu baridi

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi limeanza kusambaza misaada ya haraka na dharura kwa ajili ya kukabili msimu wa kipindi cha baridi kwa mamia ya wakimbizi walioko huko Afghanistan.

Sauti -

UNICEF yapongeza hatua ya Mexico kutenga bajeti kuwekeza watoto

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limesifu na kupongeza mpango unachukuliwa na serikali ya Mexico ambayo imeanisha shabaya

Sauti -

Watoto wazidi kusumbuliwa na utapiamlo nchini Yemen

Wafanyikazi wa kutoa misaada wanaamini kuwa idadi mpya ya watoto wanaokumbwa na utapiamlo mashariki mwa Yemen huenda ikaeleza hali ilivyo nchini humo na kupelekea wahisani kutoa misaada.

Sauti -

Bado Sri Lanka inahitaji kujiandaa kwa majanga

Miaka saba baada ya janga la Tsumani kuikumba Sri Lanka mengi bado yanahitaji kutekelezwa kwa lengo ya kuhakikisha kuwa kunatolewa onyo la mapema.

Sauti -