Viongozi wa dunia na waleta mabadiliok wanapojiandaa kukutana huko Katowice nchini Poland kwa ajili ya mkutano wa 24 wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP24, Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa itakuwa mstari wa mbele kukuletea hatua kwa hatua ya kile kinachojiri kwenye kikao hicho.
Fuatilia majadiliano na mashauriano juu ya jinsi mataifa kwa pamoja yanaweza kudhibiti ongezeko la joto duniani. Fahamu jinsi teknolojia za kisasa zaidi zilizopo zinaweza kupunguza madhara ya shughuli za binadamu kwa sayari ya dunia. Ambatana nasi ili uweze kufahamu wale ambao wanaleta mabadiliko chanya kila siku na kila wakati kote duniani.
Kupokea taarifa mpya kadri zinavyopatikana kutoka Idhaa ya Kiswahili, hakikisha unajisajili ili ufahamu zaidi kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabianchi.