Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN News

Makala Maalum

Amani na Usalama Tangazo la Marekani na Iran la sitisho la mapigano kwa wiki mbili, yatarajiwa kuwa litawezesha kufunguliwa kwa mlango wa bahari wa Hormuz, njia muhimu ambamo kwayo moja ya tano ya nishati ya mafuta na gesi duniani hupitia kwa kutumia meli.

Habari Nyinginezo

Afya Madaktari na wahudumu wa afya katika ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel wanaonya kuwa mfumo wa afya katika eneo hilo sasa uko karibu zaidi kuporomoka kuliko wakati mwingine wowote, huku idadi ya wagonjwa ikiendelea kuongezeka, magonjwa ya ngozi na ya kupumua yakienea, na uwezo wa kuwahudumia watu wenye magonjwa sugu ukiendelea kupungua. 
Utamaduni na Elimu Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa kushirikiana na  Benki ya Dunia linaendelea kurejesha matumaini ya elimu kwa maelfu ya watoto katika Jimbo la Mto Nile nchini Sudan kupitia Programu za Elimu Mbadala (ALP), baada ya miaka mingi ya vurugu na kusitishwa kwa masomo kuathiri mustakabali wao. Feissal Kirwa anaangazia zaidi.