Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN News

Makala Maalum

Wanawake Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wanawake, UN Women linapotimiza miaka 15 mwaka huu wa 2025, dunia imepiga hatua muhimu katika usawa wa kijinsia ambazo zimebadilisha maisha ya wanawake na wasichana kote duniani. Hii ni sababu ya kusherehekea, lakini harakati za kusukuma mbele usawa wa kijinsia zinapoteza mwelekeo.

Habari Nyinginezo

Ukuaji wa Kiuchumi Ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, ushirika wa wakulima wa mahindi na mtama wenye wanachama 20 katika Jimbo la Equatoria ya Kati, nchini Sudan Kusini, ulikua hadi kufikia wanachama zaidi ya 150, na hivyo kuwawezesha wanachama wengi kuongeza kipato chao na kuweza kuwahudumia familia zao kwa mara ya kwanza.
Malengo ya Maendeleo Endelevu Mkutano muhimu wa Ufadhili kwa Maendeleo uliofanyika Sevilla, FFD4 umekamilika kwa hali mpya ya azma na msisitizo wa kuchukua hatua zinazoweza kubadilisha maisha duniani kote, kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina Mohammed.