Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN News

Makala Maalum

Afya Aissata Touré, mwenye umri wa miaka 16, ndio kwanza amejifungua mtoto wake wa kwanza. Mama huyu ambaye naye ni mtoto, alikuwa na matumaini ya kjifungulia karibu na kijiji chao cha Ngouma nchini Mali, lakini mhudumu wa afya alimshauri aende hospitali kutokana na uwezekano wa kupata tatizo wakati wa kujifungua. Ilikuwa safari yenye changamoto na gharama kubwa.

Habari Nyinginezo

Utamaduni na Elimu Nigeria inapotimiza miaka 10 tangu tukio la utekwaji nyara la watoto wa kike 275 huko Chibok, kaskazini magharibi mwa taifa hilo, hadi sasa bado watoto 90 wamesalia mateka na nchi hiyo inasalia na kumbukumbu ya tukio linguine la wanafunzi wa shule kutekwa nyara jimboni Kaduna mwezi Machi mwaka huu, hali inayosababisha Umoja wa Mataifa kutoa wito mahsusi.
Amani na Usalama Leo Aprili 15, 2024 ni mwaka mmoja kamili tangu vita ya sasa nchini Sudan ilipoanza kutokana na mvutano mkali kati ya pande mbili za wanajeshi wanaohasimiana (Vikosi vya Msaada wa Haraka, RSF na Vikosi vya jeshi la Sudan, SAF katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.