Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN News

Makala Maalum

Amani na Usalama Ni miaka 30 iliyopita mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda yaliyoishangaza, kuishtua na kuitikisa duniani yalitokea kuanzia Aprili 7 mwaka 1994 na kudumu kwa siku 100 zilioghubikwa na mauji ya kikatili na watu kufurushwa makwao. 

Habari Nyinginezo

Amani na Usalama Huko ukanda wa Gaza ambako ni nusu mwaka sasa tangu mashambulizi yaanze baada ya wapiganaji wa Hamas kushambulia Israel Oktoba 7, 2024, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limetangaza kwamba moja ya magari yake lilishambuliwa kwa risasa za moto jana Jumatano wakati likisubiri kuingia kaskazini mwa Gaza kutokea kusini mwa eneo hilo.
Amani na Usalama Mshauri Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari, Alice Nderitu amesema anatiwa wasiwasi sana na kile kinachoendelea duniani kutokana na viashiria mauaji ya kimbari na iwapo dunia imejifunza kutokana na kile kilichotokea Rwanda na kule Srebrenica.