Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN News

Makala Maalum

Amani na Usalama Wakati uvamizi wa Urusi huko Bucha katika siku za mwanzo za uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine, ulimalizika mnamo Machi 2022, uharibifu mkubwa ulionekana, na tume ya Umoja wa Mataifa ikihitimisha kwamba uhalifu wa kivita ulikuwa umetendwa dhidi ya raia, miaka miwili baadaye, maisha yanarudi katika mji ulio nje kidogo ya Kyiv, ambao umerejeshwa kwa msaada wa UN.

Habari Nyinginezo

Wahamiaji na Wakimbizi Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM na wadau wake 27 wametoa ombi la dola milioni 112 ili kutoa usaidizi wa kibinadamu na maendeleo kwa zaidi ya wahamiaji milioni1.4 na jamii zinazo wakaribisha katika nchi za pembe ya Afrika, Yemen na Afrika Kusini. 
Amani na Usalama Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia watoto UNICEF na la mpango wa chakula duniani WFP leo yametoa wito wa kuchukuliwa hatua mara moja kuwalinda watoto na familia zao waliojikuta katikati ya machafuko yanayoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, huku lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR likielezea wasiwasi mkubwa kuhusu mustakbali wa zaidi ya raia milioni 7 waliotawanywa na kuomba msaada zaidi kutoka jumuiya ya kimataifa.