Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN News

Makala Maalum

Masuala ya UM Je, itachukua nini kwa Palestina kuwa Nchi Mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa? Wakati Baraza la Usalama linashughulikia suala hilo wakati vita vya uharibifu huko Gaza vikiingia mwezi wake wa saba, tuliangalia hali ya sasa ya Palestina na kile kinachohitajika kuwa Nchi Mwanachama wa Umoja wa Mataifa.

Habari Nyinginezo

Haki za binadamu Ripoti za kutisha zinaendelea kuibuka kuhusu makaburi ya halaiki huko Gaza ambako waathirika wa Kipalestina wameripotiwa kuvuliwa nguo wakiwa wamefungwa mikono, jambo ambalo limezusha wasiwasi juu ya uwezekano wa  kuweko kwa vitendo vya uhalifu wa kivita huku kukiwa na mashambulizi ya anga ya Israel yakiendelea kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR.
Haki za binadamu Wataalamu wa Umoja wa Mataifa leo Aprili 22 wameelezea wasiwasi wao kuhusu jukumu la mashirika ya ndege na mamlaka ya usafiri wa anga katika kuwezesha kuondolewa kinyume cha sheria waomba hifadhi nchini Uingereza kuelekea nchini Rwanda kwa mujibu wa Mkataba kati ya serikali ya Uingereza na serikali ya Rwanda, na Muswada wa ‘Usalama wa Rwanda’.