Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN News

Makala Maalum

Masuala ya UM Je, itachukua nini kwa Palestina kuwa Nchi Mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa? Wakati Baraza la Usalama linashughulikia suala hilo wakati vita vya uharibifu huko Gaza vikiingia mwezi wake wa saba, tuliangalia hali ya sasa ya Palestina na kile kinachohitajika kuwa Nchi Mwanachama wa Umoja wa Mataifa.

Habari Nyinginezo

Msaada wa Kibinadamu Kufuatia tamko la serikali ya Sudan Kusini la kufuta uamuzi wake wa awali wa kutoza kodi malori yenye shehena za mafuta, Umoja wa Mataifa nchini humo umesihi kuachiliwa haraka kwa malori yake yaliyosheheni bidhaa hiyo pamoja na vifaa vingine muhimu.  
Wahamiaji na Wakimbizi Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Turk na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Filippo Grandi hii leo wametoa wito kwa serikali ya Uingereza kufikiria upya mpango wake wa kuwahamishia nchini Rwanda wasaka hifadhi wanaofikia nchini humo.