Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN News

Makala Maalum

Afya Aissata Touré, mwenye umri wa miaka 16, ndio kwanza amejifungua mtoto wake wa kwanza. Mama huyu ambaye naye ni mtoto, alikuwa na matumaini ya kjifungulia karibu na kijiji chao cha Ngouma nchini Mali, lakini mhudumu wa afya alimshauri aende hospitali kutokana na uwezekano wa kupata tatizo wakati wa kujifungua. Ilikuwa safari yenye changamoto na gharama kubwa.

Habari Nyinginezo

Afya Madaktari wakuu wa Umoja wa Mataifa hii leo wamesema kuwa kuenea ulimwenguni kwa maambukizi ya ugonjwa wa  "mafua ya ndege" kwa mamalia wakiwemo binadamu ni suala muhimu la afya ya umma ambapo wametangaza hatua mpya za kuchukua kukabiliana na magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya hewa.
Afya Muungano wa chanjo duniani Gavi na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF hii leo wamekaribisha taarifa za kuidhinishwa kwa chanjo mpya ya kipindupindu iitwayo Euvichol-S ambayo ni ya matone na itapatikana duniani kote kwa bei nafuu.