Vichwa vya Habari
Chaguo la Mhariri
Makala Maalum
Amani na Usalama
Haiti inakabiliwa na ghasia zilizoenea za magenge ya uhalifu, taasisi za nchi hiyo ziko kwenye hatihati ya kuporomoka na raia wake wanakabiliwa na changamoto za kila siku za kuweza kuishi. Hata hivyo, katikati ya janga hili la usalama na kibinadamu, Umoja wa Mataifa unaendelea kutoa msaada muhimu kwa watu walioathirika.
Habari kwa Picha
Uwekezaji kwa wanawake ulivyoleta mabadiliko chanya kwenye jamii mashinani
Maudhui ya siku ya wanawake duniani mwaka huu wa 2024 ni Wekeza kwa Wanawake - Chochea Maendeleo. Maudhui haya tayari yamejidhihirisha wazi kuanzia Afrika, Asia, Mashariki ya Kati, Amerika hadi Ulaya kwani mashirika ya Umoja wa Mataifa yamebeba jukumu la kuchochea kasi ya kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kupitia wanawake. Habari Picha hii ni kithibitisho.
Habari Nyinginezo
Amani na Usalama
Mgogoro mbaya huko Gaza umeendelea, pamoja na vurugu za kila siku katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, amesema Tor Wennesland, Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Mchakato wa Amani ya Mashariki ya Kati akihutubia Baraza la Usalama leo (26 Machi) jijini New York, Marekani.
Sheria na Kuzuia Uhalifu
Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Hatua Maalum za Ulinzi dhidi ya Ukatili na Unyanyasaji wa Kingono imewekwa wazi hii leo.